Monday, 26 October 2015

CCM YASEMA IMESHASHINDA MAJIMBO 176, IMEREJESHA MAJIMBO 11



CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kimesema hadi sasa kimeshinda majimbo 176 ya uchaguzi, ikiwa ni pamoja na kurejesha majimbo 11 yaliyochukuliwa na upinzani katika uchaguzi uliopita wa mwaka 2010.

Akizungumza na waandishi wa habari leo mjini Dar es Salaam, mjumbe wa kamati ya uchaguzi ya CCM, January Makamba, amesema majimbo hayo ni kwa mujibu wa taarifa za wasimamizi wa Chama.

Aidha, Makamba ameitaka Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), kuingilia kati taarifa za matokeo feki zinazotolewa na baadhi ya mitandao ya kijamii.

Amesema taarifa nyingi zilizotolewa na mitandao hiyo hadi sasa si za kweli na zimelenga kuwavuruga wananchi na hatimaye kuzusha vurugu.

Makamba amewataka wanachama, wafuasi na wapenzi wa CCM kuwa na subira na kusubiri matokeo halali yatakayotangazwa na NEC.

No comments:

Post a Comment