Saturday, 30 April 2016
SHAKA: KATAENI SIASA ZA UKANDA NA UZAWA
Na Woinde Shizza, Mwanga
Umoja wa vijana wa Chama cha Mapinduzi umewataka wananchi wa mikoa yaKaskazini mwa Tanzania kukataa na kuzikwepa siasa za uzawa na ukanda kwa sababu ubaguzi ni dhambi isiyosamehewa na mungu.
Wametakiwa kutambua kuwa ubaguzi ni zaidi ya laana ambayo ikiemea na kujengeka katika jamii kuiondosha kwake ni kazi ngumu na kwamba
kafara yake lazima maisha ya watu yapotee au damu imwagike.
Hayo yamelezwa jana na Kaimu katibu mkuu wa UVCCM Shaka Hamdu shaka wakati akizungumza na wanachama wa CCM katika kijiji cha Mtalang’a kata
ya Mwanga mkoani hapa.
Shaka alisema ni aibu binadamu aliyestaarabika, kupata elimu akawa anaishi, kupigania madaraka., vyeo au utawala kwa kutumia maneno au sera
za ubaguzi wa dini, ukabila, uzawa au ukanda.
Aidha aliongeza kuwa baada ya miaka 52 ya uhuru na Muungamo wa mataifa ya Tanganyika na zanzibar, anapotokea kiiobgozi au chama cha siasa kinachokifanya shughuli za kisiasa kwa kueneza sumu ya uzawa na watu kupiga kura kwa
ukanda ni hatari mpya mbele ya watanzania.
“Ndugu zangu wananchi wa mikoa ya Kaskazini kuna hatari inawanyemelea, msipoitahadhari na kukwepa, ikiwaingia kutoka kwake ni mbinde, ili ifanyike kafara ya kuondoa laana hiyo si ajabu damu ikamwagika “alisema Shaka
Alisema wakati baadhi ya wananchi wa mikoa hiyo wakiaza kughilibiwa na wanasiasa uchwara wakubali kuchagua vyana kwa sababu za ukanda na ukabila, idadi kubwa ya wakaazi wa mikoa hiyo wanaishi na wamejijenga kiuchumi katika mikoa mingine ya nchi na huko hawabughudhiwi wala kubaguliwa.
“Haiikisha mkiendela kubagua wenzetu na nyinyi mtaanza kubaguliwa,vdhambi ya ubaguzi haina toba, kataeni siasa chafu na wakwepeni matapeli wa kisiasa na walafi wa madaraka “alisisitiza shaka.
Kaimu huyo katibu mkuu wa UVCCM alisema kwamba Taifa la Tanzania halikuachwa na wakoloni bali liliundwa na waasisi wake Marehemu baba wa
Taifa Mwalimu julius Nyerere na Hayati Mzee Abeid Amani Karume bila na kupiga vita ubaguzi wa kikabila, udini, rangi za watu au kuendekeza
uzawa.
Alisema kutendo chochote kitakachopelekea kuacha au kuipuuza misingi ya Taifa letu ambayo imewafanya watu kuwa na umoja, upendo na
mshikamano radhi za waasisi hao pamoja na za wenzao zitaigeukia nchi yetu iwapo tutakubali kugawanywa na wanasiasa wachovu.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa uvccm mkoa wa Kilimanjaro Juma Raib Juma alisisitiza haja ya kuendelea kuheshimu na kudumisha umoja wa kitaifa
nchini na mwanasiasa yeyote atakayeonekaa kana ni mkabila, mdini na asiyehimiza amani na utulivu aogopwe kama ebola.
“Ni mkoa upi leo hii nchini kwetu ambao wanaishi janii ya watu wa kabila moja,dini moja,rangi moja au ukoo mmoja,tikate ukabila na vyama vilivyoanza kuonyesha ubaguzi wa aina yeyote, “alisema Raibu
Mwenyekiti huyo wa UVCCM mkoani kilimanjaro alisema vyama vinavyopita na kueneza siasa za chuki, ukanda au ukabila vichunguzwe na ikiwa
vitawajibika kujihusisha na vitendo hivyo hatari Msajili wa vyama vya siasa nchini achukue hatua za kisheria kuifuta mara moja kabla havijaleta madhara.
Shaka na msafara wake wanaendelea na ziara katika wilaya ya Mwanga kabla ya kuhitimisha wilaya ya Same baadae kuelekea mkoani Tanga.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment