NA NJUMAI NGOTA
MGOMBEA mwenza wa urais wa
Chama Cha Mapinduzi (CCM), Samia Sululu Hassan, amesema hatishwi na watu
wanaohamia vyama vya upinzani kwa sababu anachokiona ni chama kilekile
kinachogombea upande wa pili.
Amesema kile
kinachogombewa upande wa pili amekibatiza jina la CCM maslahi kikichuana dhidi
ya CCM halisi, jambo linaloweka uwazi wa msimamo sahihi ulikosimamia kuwa ni
CCM halisi ambayo yeye anapeperusha bendera yake.
Samia alisema hayo juzi,
usiku alipokuwa akihojiwa katika kipindi cha The Mboni Show kinachorushwa na
Shirika la Utangazaji la Tanzania (TBC1).
Mgombea huyo alisema watu
wanaohamia vyama vya upinzani wamekuwa ndani ya Chama kwa muda mrefu na
wametumika nafasi mbalimbali ndani ya Chama na wengine walikuwa mawaziri na
manaibu.
“Sasa kinachotokea ni
hiki, mimi hakinitishi sana kwa sababu nachokiona ni CCM ile ile inayogombea
kuna wale CCM halisia wagombea upande
mmoja na CCM maslahi wamenunua chama ili
wagombee upande mwingine,”alisema.
Alisema Umoja wa Katiba wa
Wananchi (UKAWA), haoni kwa sababu
waanzilishi wa umoja huo akiwemo
Profesa Ibrahim Lipumba ameona misingi yake imekiukwa na kusema anatoka kwa mujibu wa maneno yake.
Samia kwa upande wake Dk.
Willbroad Slaa naye yupo kimya na hawafahamu anachofanya lakini waswahili
wanasema kimya kingi kina kishindo.
Alisema hao CCM maslahi
walionunua chama ni wanaCCM kwa hiyo aliwahakikisha kuwa Chama kitashinda kwa
kishindo kubwa katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25, mwaka huu.
No comments:
Post a Comment