Na Mwandishi Wetu, Njombe
UMOJA wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), umesema uchaguzi mkuu wa nchi ni zaidi ya vita na kwamba jukumu walililonalo vijana wa CCM ni kushinda kwa nguvu ya hoja na mikakati.
UVCCM, imewataka vijana kujivunia mafanikio yaliopatikana chini ya Rais Jakaya Kikwete na kuyafanya kuwa kigezo cha kuiombea kura katika uchaguzi mkuu wa Oktoba 25, mwaka huu.
Kauli hiyo ilitolewa jana na Kaimu Katibu Mkuu wa UVCCM
Taifa, Shaka Hamdu Shaka, alipokutana na wajumbe wa Kamati ya Utekelezaji ya
UVCCM Wilaya ya Njombe, mkoani hapa.
Alisema vita ya uchaguzi ni shughuli inayohitaji kupata
wapiganaji walioandaliwa kifikra, kifalsafa na kiitikadi na kwamba si jambo la kukurupuka kama vifanyavyo vyama vya upinzani vinavyofikiri kushika dola ni jambo legelege.
"Mafanikio ya serikali yetu chini ya Rais Kikwete
na bidii ya kila mwana-CCM, kwa kutumia juhudi, maarifa na dhamira, vinapaswa
kuzingatiwa ili kushinda vita iliyo mbele yetu," alisema.
Aliwahimiza viongozi wa UVCCMmkoani Njombe, kuhakikisha kila mmoja anatimiza wajibu wake katika dhamana aliyokabidhiwa bila kukawia, kuzembea au kutegeana.
Aidha, aliwataka watendaji wa jumuia hiyo kutumia muda kidogo kubaki ofisini na muda mwingi wautumie kufanikisha malengo waliyojiwekea.
"Nimeridhika na kujipanga kwenu, sasa ingieni
kwenye uwanja wa vita mkijiamini na kurudi na ushindi. Watanzania wanamhitaji Dk. John Magufuli awaongoze
kwa sababu si fisadi, bepari wala hana udokozi wa mali za umma," alisema.
Shaka alisema utendaji unaoonekana katika kila kona ya
Tanzania katika miaka 10 ya uongozi wa Rais Kikwete ni mtaji mnono wa kuipatia
ushindi CCM.
Kwa upande wake, Katibu wa UVCCM Mkoa wa Njombe, Consolata Msembele, alimhakikishia Shaka kwamba mkoa wake umejipanga kimkakati kukikiltea Chama ushindi utakaomuweka madarakani mgombea urais wa CCM, wabunge na madiwani.
Kwa upande wake, Katibu wa UVCCM Mkoa wa Njombe, Consolata Msembele, alimhakikishia Shaka kwamba mkoa wake umejipanga kimkakati kukikiltea Chama ushindi utakaomuweka madarakani mgombea urais wa CCM, wabunge na madiwani.
Consolata aliongeza kwamba UVCCM wako imara, makini, wasioyumbishwa au kustushwa na baadhi ya viongozi wastaafu akiwemo Waziri Mkuu aliyejiuzulu kwa kashfa ya Richmond, Edward Lowassa, Waziri Mkuu mstaafu, Frederick Sumaye na baadhi ya waliokuwa wana-CCM walioshika nafasi mbalimbali serikali, ikiwemo uwaziri, Joseph Mungai, Lawrence Masha na Makongoro Mahanga waliohamia upinzani.
"Lowassa na Sumaye wameikuta na kuiacha CCM iko na uimara wake ule ule, nafikiri wamejipotezea hadhi, staha na heshima waliyokuwanayo kwa kuwa hawakujipima kabla ya kuamua kuhama Chama," alisema.
Shaka na msafara wake jana walianza ziara ya kampeni
mkoani Njombe, ambako alipokelewa na uongozi wa UVCCM wa mkoa huo katika kijiji
cha Idofi.
Akiwa mkoani humo, anatarajiwa kushiriki katika shughuli mbalimbali za kisiasa, ikiwemo kuhutubia mikutano ya hadhara ya kumnadi mgombea urais wa CCM, Dk. John Magufuli, wabunge na madiwani kabla ya kuendelea na ziara yake katika mikoa ya Ruvuma, Singida, Mwanza, Simiyu, Mara, Dar es Salaam, Pemba na Unguja.
No comments:
Post a Comment