Tuesday 3 November 2015

BREAKING NEWS TB JOSHUA ATUA DAR LEO, KUSHUHUDIA KUAPISHWA KWA MAGUFULI KESHOKUTWA

RAIS Jakaya Kikwete akizungumza na TB Joshua, alipomtembelea leo Ikulu, Dar es Salaam
RAIS Kikwete alisalimiana na TB Joshua
Mtume TB Joshua wa Kanisa la Church of All Nations la nchini Nigeria, ametua Jijini Dar es Salaam leo, kwa ajili ya kuja kushuhudia kuapishwa kwa Rais wa Awamu ya Tano Dk. John Pombe Magufuli.

Mara baada ya kutua kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar es Salaam, TB Joshua alikwenda moja kwa moja  Ikulu, kumsalimia Rais Jakaya Kikwete.

Katika mazungumzo yao, TB Joshua alimpongeza Rais Kikwete kwa kufanikisha uchaguzi mkuu wa rais, wabunge na madiwani, uliofanyika Oktoba 25, mwaka huu, ambao alisema ulifanyika kwa uhuru na amani.

Alimweleza Rais Kikwete kuwa, kutokana na kufanikisha uchaguzi huo, anaondoka madarakani kwa furaha na amani.

Aidha, alimpongeza Rais Kikwete kwa kukiwezesha Chama Cha Mapinduzi (CCM), kumpata Dk. Magufuli kuwa raia wa awamu ya tano.

Alimwelezea Dk. Magufuli kuwa ni Rais wa Baraka na Fanaka tele katika awamu hii mpya.

No comments:

Post a Comment