Thursday 12 November 2015

WANACHAMA SABA ZAIDI WA CCM WACHUKUA FOMU KUWANIA USPIKA

NAIBU Spika Job Ndugai (kulia) akipokea fomu ya kuwania uspika kutoka kwa Muhammed Seif Khatin jana
DIDAS Massaburi naye akipokea fomu
GODBLESS Blandes akipokea fomu
RITA Mlaki akipokea fomu
VARAIKUNDA Urio naye akichukua fomu
PHILIP Marko naye ndani
Mzee Samuel Sitta alichukua fomu jana

WANACHAMA saba zaidi leo wamechukua fomu za kuomba kuteuliwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa ajili ya kuwania Uspika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano.

Waliochukua fomu leo ni pamoja na Naibu Spika wa Bunge hilo, anayemaliza muda wake, Job Ndugai.

Wengine ni Julius Pawatila, Dk. Tulia Arkson, Dk. Medadi Majogolo Kalemani, Dk. Didas Masaburi, mbunge wa zamani wa jimbo la Kawe, Ritta Mlaki na Veraikunda Urio.

Makada hao wanaungana na wenzao 10 waliochukua fomu jana, ambao ni  Waziri wa Uchukuzi, Samuel Sitta, aliyekuwa mbunge wa Karagwe,Gosbert Blandes,Leonce Mulenda, George Nangale, Profesa Costa Mahalu, Muzamil Kalokola, Banda Sonoko,Simon Rubugu na Dk. William Nchimbi.

No comments:

Post a Comment