Monday, 21 December 2015

ORODHA YA WAUZA DAWA ZA KULEVYA HAINISADII-KITWANGA


Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (kushoto) akisalimiana na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Ernest Mangu wakati alipokuwa anawasili Makao Makuu ya Jeshi hilo, jijini Dar es Salaam kwa ziara ya kikazi. Waziri Kitwanga alifanya mazungumzo na Viongozi Wakuu wa jeshi hilo na kukubaliana kuweka mikakati zaidi ya kukabiliana na uhalifu nchini.
Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii

WAZIRI wa Mambo Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga amesema njia ya kudhibiti dawa za kulevya kuingia nchini ni kuweka mfumo wa kisasa wa kudhibiti uingiaji dawa hizo, kuwa na orodha ya waingizaji wa dawa ni kazi bure kutokana na kukosa mamlaka ya kisheria.
 
Kitwanga ameyasema hayo leo jijini Dar es Salaam wakati alipokutana na Maafisa Wakuu wa Jeshi la Polisi, amesema katika kukabiliana na uingizaji wa dawa za kulevya ni kuweka mfumo imara na jeshi la polisi lazima lijipange katika udhibiti huo.
 
Kitwanga amesema kuwa mfumo wa kiteknolijia ukiwekwa hautabagua mtu yeyote au mkubwa katika madaraka awe mdogo wakishajulikana watachukuliwa hatua za kisheria bila kuangaliwa nafasi walizo nazo.
 
“Orodha ya wauza unga ukiwanayo haitasaidia na kufanya hivyo ni kuhisi, lakini huna sheria ya kuweza kuwabana katika orodha hiyo” amesema Kitwanga.
 
Kitwanga amesema kuwa katika mambo waliyojpanga nayo na jeshi la polis ni kuhakikisha wanaimarisha ulinzi katika bandari ili kuweza kudhibiti utoroshaji wa vitu mbalimbali ambavyo vinatoka bila utaratibu.
 
Hata hivyo amewataka polisi watu washitakiwe kwa kesi walizo nazo na sio kuwabambikia watu wasio na hatia kusababisha kufungwa kwa kesi zisizowahusu.
 
Kitwanga amesema utoroshaji wa madini,jeshi la polisi haliwahusu wakihitajika na Wizara ya Nishati na Madini watafanya hivyo katika kukabiliana na utoshaji huo.
 
Aidha amesema kati ya askari 45,000 ni askari 10,000 ndio wenye makazi hivyo wanatarajia kujenga nyumba 5000 ikiwa nia nia askari wote kukaa katika makambi ni rahisi kuweza kuhitajika kwa muda wowote.

No comments:

Post a Comment