Tuesday, 26 January 2016

LUKUVI AWAAGIZA WATENDAJI WA HALMASHAURI YA MANISPAA YA ILALA NA SHIRIKA LA NYUMBA LA TAIFA KUBOMOA JENGO HILI NDANI YA MWEZI MMOJA

Jengo refu lilojengwa chini ya kiwango lililopo katika mtaa wa Indiraghandi jijini Dar,kama lionekanavyo pichani.
Sehemu ya jengo ambayo inaonekana imepasuka.Picha na Emmanue Massaka wa Globu ya jamii
WAZIRI wa Nyumba, Ardhi na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi amewaagiza watendaji wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala na Shirika la Nyumba la Taifa kubomoa jengo refu lilojengwa chini ya kiwango lililopo katika mtaa wa Indiraghandi ndani ya mwezi mmoja kuanzia sasa.
 

Lukuvi ametoa kauli hiyo jijini Dar es Salaam kabla ya kuelekea kwenye ziara fupi katika Wilaya ya Bagamoyo Mkoani Pwani ambapo nako pia amebaini matatizo mbalimbali katika sekta  ya Ardhi.
 

“Miezi sita iliyopita Rais Mstaafu alikuja hapa akaagiza jengo hili libomolewe na nyie mkajiridhisha kweli lafaa kubomolewa sasa inakuwaje mpaka leo linaendelea kuwepo, hivyo naagiza mfanye haraka jengo hili ndani ya mwezi mmoja taratibu za ubomoaji ziwe zimeanza ili kulinusuru taifa kuingia katika janga jingine.”alisema Waziri Lukuvi.
 

Akiwa bagamoyo waziri Lukuvi alibaini katika Wilaya ya Bagamoyo upotevu wa viwanja  vya wanachi ambavyo walitakiwa kupewa katika eneo la ukuni ambapo vimetoweka
 

Mara baada ya kupata taaarifa hiyo mmoja wa wakaazi wa bagamoyo ambaye alitoa malalamiko juu ya viwanja hivyo mbele ya mkutano wa hadhara na kutaja kuwa Halmashauri ilichukua kiasi cha pesa kuanzia laki sita kwa kila mtu mwaka 2005 na kuahaidi kuwapatia viwanja lakini mpaka leo hawajapewa.
 

Mara baada ya kupata taarifa hiyo waziri Lukuvi aliwagiza watendaji wa wilaya hiyo ndani ya miezi sita wawe wamewapatia wakazi hao viwanja hivyo.

No comments:

Post a Comment