Friday, 29 January 2016

NAPE ATAKA BUSARA ITUMIKE UKOSOAJI WA SERIKALI


SERIKALI imevihakikishia vyombo vya habari kuwa ipo tayari kukoselewa, lakini wakosoaji wake wanatakiwa kutumia busara na njia sahihi katika kufi kisha ujumbe pasipo kuvunja sheria zilizopo.

Hayo yameelezwa jana na Waziri wa Habari, Utamaduni, Wasanii na Michezo, Nape Nnauye , wakati akifungua mkutano mkuu wa Jukwaa la Wahariri wa Vyombo vya Habari Tanzania (TEF) unaoendelea mjini hapa.

Alisema amelazimika kutoa kauli hiyo kutokana na kusambaa kwa dhana potofu kuwa, serikali haipo tayari kukosolewa, jambo alilosema si kweli na kusisitiza serikali ipo tayari wakati wote kukoselewa.

Alisema  dhana hiyo imetokana na hatua yake ya kulifungia gazeti la Mawio pamoja na uamuzi wa kubadilisha ratiba ya urushaji wa matangazo ya Bunge kwa Televisheni ya Taifa (TBC), kitendo ambacho kilipingwa vikali na wabunge.

Nape alisema ni kweli kwamba baadhi ya sheria zinazotumika sasa zimepitwa na wakati, bali zinatumika kwa sababu hakuna sheria nyingine.

Alisema ili sheria hizo zilizopitwa na wakati ziache kutumika, ni lazima juhudi za haraka zifanyike kuzibadilisha ili kuwe na uhuru wa vyombo vya habari.

Alisema sera iliyopendekezwa na vyombo vya habari ni nzuri, lakini imekuwa ikikinzana na sheria zilizopo, hivyo ni vyema wadau wote wakahakikisha vinaenda sambamba.

Awali, Mwenyekiti wa TEF, Absalom Kibanda, alisema kuwa Waziri Nnauye ni mmoja wa viongozi walio karibu na vyombo vya habari katika kuhakikisha muswada wa vyombo vya habari unaboreshwa.

Hata hivyo, alimtaka Waziri huyo kufi kisha ombi lao kwa Dk. John Magufuli ya kuwa na utaratibu wa kukutana na wahariri kila mwezi ili kuzungumzia masuala mbalimbali yanayohusu nchi.

No comments:

Post a Comment