Tuesday 22 March 2016

CHADEMA YATWAA KITI CHA UMEYA DAR



KAIMU Mkurugenzi Jiji  la Dar es Salaam Bi. Sara Yohana amemtanganza Isaya Chacha Diwani wa Kata ya Vijibweni  (CHADEMA) kutoka Wilaya ya Temeke kuwa Meya wa Jiji la Dar es Salaam mara baada ya uchaguzi.

Kaimu Mkurugenzi huyo alisema hayo mara baada ya uchaguzi uliyofanyika leo  jijini Dar es Salaam, ambapo mshindi alipata kwa kura 84 dhidi ya mgombea kupitia chama cha CCM
Bw.Yenga Yusuph ambaye alipata kura 67. Katika uchaguzi huo kura 7 ziliharibika.

“Tunawashuruku wapiga kura wote mlioshiriki zoezi hili la upigaji kura kwa utulivu bila vurugu na kuweza kulifanikisha mpaka kumpata Meya wa Jiji hili,” alisema Bi. Yohana.

Kwa upande wa mshindi wa kiti hicho, Chacha alisema anawashukuru wapiga kura wake wa kata ya Vijibweni kwa kumchagua kuwa diwani pamoja uongozi wa chama chake kwa kukubali kumpa nafasi ya kugombea kiti hicho.

“Nimejipanga kuleta maendeleo katika sekta ya elimu pamoja na kupambana na kero ya foleni katika jiji pia hakikisha wananchi wote maskini wanafaidika  na mapato ya jiji hili katika kuendeleza miundombinu mbalimbali ,”alisema Chacha.

Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo, Freeman Mbowe alisema idadi ya wapiga kura tu inaonyesha wazi kuwa ushindi wa kiti hicho cha meya ni lazima uchukuliwe na  CHADEMA sababu  madiwani wengi wa mkoa wa Dar es Salaam wanatoka katika chama hicho.

No comments:

Post a Comment