Na Rashid Zahor, Mwanza
MGOMBEA urais wa CCM, Dk. John Magufuli, amekiri kuwa tangu alipoanza kufanya mikutano ya kampeni Agosti mwaka huu, hajawahi kupata mapokezi makubwa kama aliyoyapata jana mjini Mwanza.
"Mwanza mmefunika kweli kweli. Sijawahi kupata mapokezi makubwa na ya aina yake kama haya ya Mwanza. Nadhani mnaweza kuongoza Afrika," alisema Dk. Magufuli alipokuwa akihutubia mkutano wa kampeni, uliofanyika kwenye viwanja vya Furahisha, jijini hapa.
"Sijawahi kuona watu wakijitolea kutembea kwa miguu umbali wa kilometa 12 kutoka uwanja wa ndege hadi mjini. Nina deni kubwa la kufanya kwenu. Nalo ni kuwafanyia kazi. Hapa kwangu kazi tu," alisema Dk. Magufuli huku akishangiliwa na wananchi kwa mayowe mengi.
Kutokana na mapokezi aliyoyapata Mwanza na yale aliyoyapata Zanzibar, Dk. Magufuli alisema sasa ana uhakika wa kushinda urais kwa asilimia 99 na kwamba ana imani kubwa atakuwa Rais wa Tanzania.
Mapokezi aliyoyapata Dk. Magufuli yameelezewa kuwa yameandika historia mpya katika Jiji la Mwanza, yakiwa yamevunja rekodi ya yale aliyoyapata mgombea urais wa CHADEMA, Edward Lowassa, aliyefanya mkutano wake mjini hapa mwanzoni mwa wiki hii.
Aidha, kutokana na kufurahishwa na mapokezi hayo, Dk. Magufuli aliwaahidi wananchi wa Mwanza kwamba ataligeuza Jiji hilo kuwa Geneva ya Afrika kimaendeleo.
"Mmekusanyika hapa bila kubagua vyama. Mmekuja kwa umoja wenu. Hapa wapo CUF, CHADEMA na CCM, kwangu wote ni sawa kwa sababu nikichaguliwa kuwa rais, nitakuwa rais wa Tanzania," alisema.
Mgombea huyo wa urais wa CCM, aliwahoji wananchi hao iwapo kuna mgombea mwingine wa urais kutoka vyama vya upinzani, aliyewahi kupata mapokezi kama aliyoyapata yeye na kujibiwa hakuna.
Dk. Magufuli alianza kuhutubia mkutano huo saa 10:02 jioni na kumaliza saa 11:50. Alihutubia kwa zaidi ya saa moja na nusu, ikiwa ni rekodi yake mpya ya kuhutubia mkutano wa kampeni kwa muda mrefu zaidi.
Aliwaeleza wananchi wa Mwanza kwamba serikali yake imepania kufanya mabadiliko ya kweli ya kwenda mbele na pia kuwaondolea umasikini wananchi kutoka kiwango cha sasa cha asilimia 28.2.
Mgombea huyo ambaye amejielezea kuwa ni waziri pekee aliyekaa kwenye wizara moja kwa miaka 12, aliwaahidi wananchi wa Mwanza kuwa, serikali yake itajenga barabara za watembea kwa miguu kwenye eneo la uwanja wa Furahisha zitakazoligeuza eneo hilo kuwa la utalii.
"Fedha zipo, zimeshatengwa na ujenzi utaanza ndani ya miezi miwili,"alisema Dk. Magufuli.
Aidha, aliwaahidi wananchi hao kuwa serikali yake itanunua meli mbili za abiria kwa ajili ya usafiri wa Ziwa Victoria na meli nyingine mbili kwa ajili ya kubeba mizigo.
Pia aliahidi kujenga barabara ya Usagara/Kisesa kwa kiwango cha lami pamoja na kupanua zile za maeneo ya mjini.
Mgombea huyo pia aliahidi kujenga daraja refu kuliko yote nchini kutoka Kidongo hadi Busisi na kuongeza kuwa michoro ya daraja hilo itaanza kufanyiwa kazi mwaka huu.
Pia aliahidi kurejesha serikalini kiwanda cha ngozi kilichoko mjini Mwanza, iwapo mmiliki wake atashindwa kukiendeleza kabla hajaapishwa kuwa rais.
Dk. Magufuli pia aliahidi kuimarisha sekta ya uvuvi na kuimarisha ulinzi katika Ziwa Victoria ili wavuvi waweze kufanyakazi bila vikwazo au kuhatarisha usalama wa maisha yao.
SHAMRASHAMRA ZA MAPOKEZI
Mji wa Mwanza ulianza kutawaliwa na pilikapilika na shamrashamra za mapokezi ya Dk. Magufuli kuanzia mapema asubuhi, wakati waendesha bodaboda waliokuwa wamezipamba pikipiki zao kwa bendera za Chama walipokuwa wakiziendesha kwa mbwembwe barabarani.
Aidha, katika maeneo mbalimbali, vijana walikuwa wakisalimiana kwa maneno ya 'Hapa Kazi tu', kuashiria kaulimbiu ya mgombea urais wa CCM, ambaye ni mchapakazi asiye na mfano.
Viwanja vya Furahisha vilianza kufurika kuanzia saa tatu asubuhi na hadi saa sita mchana, hakukuwa na mahali pa kusimama.
Nyimbo za CCM, hasa ule wa kikundi cha Tanzania One Theatre (TOT), 'Hatunywi sumu hatujinyongi', zilisikika katika maeneo mbalimbali ya Jiji la Mwanza na kuifanya siku ya jana ionekane kuwa maalumu kwa ajili ya Dk. Magufuli na chama chake.
Kwenye uwanja wa ndege wa Mwanza, wananchi walifurika kuanzia saa nne asubuhi, wakiwa wamevalia sare za CCM. Wananchi hao pia walianza kujipanga kwenye barabara ya kutoka mjini kwenda uwanja wa ndege wa Mwanza kuanzia saa nne.
Ndege iliyombeba Dk. Magufuli ilitua kwenye saa 8:23 mchana na kupokewa na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Magesa Mulongo, Mwenyekiti wa CCM Mkoa, Anthony Diallo na Katibu wa CCM Mkoa, Miraji Mtaturu, na baadaye kuanza safari ya kwenda mjini.
Kutokana na wingi wa watu waliokuwa na kiu ya kumwona, wakiwa wamesimama kando ya barabara, Dk. Magufuli alilazimika kusimama juu ya gari lake kuanzia uwanja wa ndege hadi kwenye viwanja vya Furahisha.
Polisi wa usalama barabarani na wale wa kawaida, walilazimika kufanya kazi ya ziada kuwazuia wananchi kulisogelea gari la Dk. Magufuli kabla ya kuzidiwa nguvu na kuwalazimisha walinzi wa mgombea huyo kushuka na kuwaondoa wananchi hao mbele ya gari hilo.
Mama mmoja alifanya kibweka cha aina yake baada ya kujitokeza ghafla mbele ya gari la Dk. Magufuli na kuanza kupiga push-up. Ilibidi walinzi wa mgombea huyo washuke kwenye gari na kumwondoa ili msafara uendelee.
Muda wote, wakati msafara wa Dk. Magufuli ukienda mjini, wananchi walikuwa wakiimba nyimbo za kuisifu CCM na kumtaja mgombea huyo kuwa ndiye rais wa awamu ya tano.
Katika baadhi ya maeneo, kina mama walitandika kanga kwenye barabara ili gari la Dk. Magufuli lipite juu yake. Wengine walikuwa wakisafisha barabara kwa mafagio na kupiga deki kwa maji. Polisi walikuwa na kazi ngumu ya kuwazuia.
Wingi wa wananchi waliokuwa wamesimama barabarani, ulimfanya Dk. Magufuli asimamishe msafara wake eneo la Pansiasi na kuwahutubia. Lakini badala ya kumsikiliza, wananchi hao walilipuka mayowe ya 'rais, rais, rais'.
Akiwahutubia wananchi hao, Dk. Magufuli alisema hajawahi kupata mapokezi makubwa tangu alipoanza mikutano yake ya kampeni kama ilivyokuwa kwa Mwanza.
Aliwaahidi wananchi hao kuwa kutokana na kufurahishwa na mapokezi hayo ataligeuza Jiji la Mwanza na kulifanya liwe Geneva ya Afrika kimaendeleo.
Wingi huo wa wananchi barabarani, ulimfanya Dk. Magufuli asimamishe msafara wake mara mbili na kuwahutubia ili kukata kiu ya kutaka kumuona na kumsikiliza. Kama ilivyokuwa awali, wananchi hao waliendelea kumshangilia kwa kumwita rais.
Msafara wa Dk. Magufuli uliwasili viwanja vya Furahisha saa 9:23, alasiri na kuwafanya wananchi walipuke kwa mayowe ya kumshangilia. Viwanja hivyo vilijaa pomoni na hakukuwa na sehemu ya kusimama. Wananchi wengi walilazimika kusimama mbali na viwanja hivyo huku wengine wakiwa wamepanda juu ya soko la Rock City Shooping.
Wakati mkutano wa Dk. Magufuli ukiwa unaendelea, baadhi ya wananchi walikuwa wakikimbia mchakamchaka pembeni mwa viwanja, huku wengine wakiwa wamebeba mfano wa jeneza lililokuwa na rangi za CHADEMA.
"Tumekuja wenyewe, hatukusombwa," waliimba wananchi hao.
Kutokana na wananchi wengi kuhamasika kumsikiliza mgombea huyo, shughuli katika jiji la Mwanza, zilisimama kwa muda, huku maduka na ofisi nyengine zikifungwa.
Msafara wa Dk. Magufuli, uliongozwa na zaidi ya pikipiki 1,000, kutoka uwanja wa ndege mpaka Furahisha.
Wananchi waliokuwa maeneo ya Kona ya Jeshi, Ilemelala, Sabasaba, Butuja, Iloganzala na Pasiansi walifunga barabara kushinikiza mgombea huyo awahutubie, ambaye aliwahutubia.

No comments:
Post a Comment