Saturday, 7 May 2016

TRA YAKUSANYA MAPATO YA SH.TRIRIONI 1.035 MWEZI ULIOPITA


Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii.

MAMLAKA ya Mapato Nchini  (TRA)  kwa mwezi uliopita imekusanya Sh.Trioni 1.035   ambayo ni sawa na asilimia 99.5  ya lengo  kukusanya sh.trioni 1.040 .

Akizungumza  na waandishi wa habari  jijini Dar es Salaam, Kamishina Mkuu wa TRA, Bw. Alphayo Kidata amesema kuwa katika makusanyo ya miezi  10  wameweza kukusanya sh. Trioni 10.92  ambayo sawa na asilimia 99 ya lengo ya sh.trioni 11.02  katika lengo la kipindi hicho.

Amesema kuwa  TRA imedhamiria  kukusanya zaidi ya sh. Trioni 1.4 na kuvuka
lengo la mwaka wa fedha wa 2015/2016 katika miezi miwili ya kumaliza mwaka wa fedha
ambalo ni sh. Trioni 12.3.

Bw. Kidata amesema kuwa TRA itaendelea na jitihada mbalimbali kuhakikisha  inafikia lengo la makusanyo kwa mwaka wa fedha 2015 / 2016 licha kuwepo kwa changamoto ambazo wamekuwa wakikabiliana nazo.

Amesema kuwa wananchi wamejua umuhimu wa kodi na kuanza kutoa ushirikiano katika kudhibiti mianya ya magaendo, pamoja na kuziba mianya ya upotevu wa mapato ikiwa katika usimamizi wa mifumo ya mlipa kodi kulipa kodi anayostahili bila usumbufu
wowote.

Kamishina Mkuu amesema kuwa wamewakamata wafanyabiashara 300 kwa kuwatoza faini zaidi ya sh. Milioni 746 kwa makosa ya kutotoa risti, kutoa risti zenye bei pungufu pamoja na kutotumia mashine za Kieletroniki  na baadhi yao walihukumiwa kifungo au kulipa faini .

"TRA haitawavumilia wafanyabiashara wanayoikosesha serikali mapato kwa kuuza na kutoa huduma bila risti kwa makusudi yao kamwe hawataachwa", alisisitiza Bw. Kidata.

No comments:

Post a Comment