Saturday 16 July 2016

VIGOGO WENGINE WASIMAMISHWA JESHI LA POLISI



KATIBU Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira, amewasimamisha kazi watumishi watatu wa Jeshi la Polisi kwa tuhuma za kufanya malipo hewa kwa kulipa posho ya chakula kwa watu ambao si askari.

Hatua ya kusimamishwa kazi ni  mwendelezo wa uchunguzi wa tuhuma za kufanya malipo hewa ya sh. 305,820,000 zilizosababisha kusimamishwa kazi kwa Mhasibu Mkuu wa Jeshi la Polisi, Frank Msaki, wiki iliyopita.

Waliosimamishwa ni  Damian Bupamba ambaye ni  Mhasibu Daraja la Pili, Ida Moyo ambaye ni Mhasibu Daraja la Kwanza na Mkaguzi Msaidizi wa Jeshi la Polisi, Milambo Milambo kwa  makosa ya kufanya malipo ya posho ya chakula kwa watu  wasiostahili kwa kipindi cha kuanzia mwaka wa fedha 2013/2014 hadi 2015/2016.

Taarifa iliyotolewa jana kwa vyombo vya habari na Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, ilisema watumishi hao walisimishwa kuanzia Jumatano iliyopita.

Ilisema watumishi hao walihusika  kufanya malipo hayo jambo ambalo ni kinyume na kanuni.

"Katibu Mkuu amewasimamisha wahusika hao ili kupisha uchunguzi wa tuhuma dhidi yao unaofanyika kufuatia uchunguzi maalamu wa Mkaguzi wa Ndani wa Jeshi la Polisi  uliobaini makosa ya malipo hewa.

No comments:

Post a Comment