Wednesday, 17 August 2016
TAARIFA YA UVCCM KWA WAANDISHI WA HABARI
Baina ya tarehe 12 na 16 Agosti mwaka huu mtu mmoja anayejiita kada na mwanachama wa CCM amekutana na vyombo vya habari pia akasambaza taarifa yake katika mitandao ya kijamii akielezea msuala kadhaa ya Chama Cha Mapinduzi na Jumuiya zake lakini zaidi akionekana kwa dhamira na makusudi bayana akiilenga Jumuiya ya Umoja wa Vijana ya CCM huku akiwa hana nguvu ya hoja.
Kwanini tunasema hakuwa na nguvu ya hoja zaidi ya kubwabwaja kichwa mchungwa kuliko uthabibiti wa matamshi yake katika kujenga hoja zenye mantiki, ushahidi, kuwa na maana au mashiko ili kuyapa nguvu madai yake na uthibitisho kamili juu ya anachokisema huku akiitaja UVCCM.
Kama kweli ni mwanaccm au mwana jumuiya au ni mtendaji dhamana wa jumuiya yetu, alipaswa kufuata taratibu na si kama alivyoamua kujipa dhamana bandia ya kuupotosha umma kwa kupiigania maslahi binafsi ya tumbo lake.
Aidha sote kama tujuavyo ni kwamba Chama Cha Mapinduzi na Jumuiya zake zimeundwa kwa mujibu wa Katiba, Kanuni na taratibu zake husika .Uamuzi wa kiongozi au mwanachama kusimama hadharani na kukishambulia Chama au jumuiya hasa katika masuala mazito ya ufisadi ni jambo linalohitaji kwanza mtoa hoja awe na ushahidi wa kutosha, vielelezo na viambatanisho vya madai yake .
Ikiwa kila mwanachama akiamua akimua kuamka kitandani , kujipachika wadhifa wa ukada baadae akakukutana na wanandshi wa habari kutoa shutuma, lawama na tuhuma , huo si mfumo bora na utaratibu wa chama chetu wala jumuiya zake.
Matamshi ya mtu aliyejiita kada yanayomtaka Mwenyekiti wa CCM na Rais Dkt. Magufuli aunde Tume ya Uchunguzi wa Mali za Jumuiya ya Umoja wa Vijana kwani Hali yake ni Mbaya Juu ya Mambo yafuatayo
1. Mapato ya Jengo na Juu ya Matumizi ya Fedha zinazopatikana na Mapato hayo ikiwa ni Mradi mkubwa wa Jumuiya ya Vijana (UVCCM ).
2. Minada Holela ya Mali za Chama ikiwemo Magari n.k.ambayo imekua ikifanyika kinyume na Taratibu.
3.Uhakiki wa mali za jumuiya katika miradi ya Gymkhana na Darajani zanzibar
4.Kushughulikia Wasaliti ndani ya Chama na Jumuiya yetu ya UVCCM ambao wamekua mchana CCM usiku vyama vya upinzani.
Kimsingi madai yote haya ni mazito mno, kutokana na unyeti pia uzito tuhuma husika, watu wengi walitegemea kama kweli angekuwa ni muungwana, kwanza angefuata utaratibu na angeonyesha ushahidi , vielelezo au viambatanisho vya tuhuma hizo moja baadae ya moja kwasababu madai hayo ni mzingo wa jinai.
Ninachokisema ni kwamba chama chetu na jumuiya zake zimeundwa kwa taratibu halali na husika za katiba , viongozi wa jumuiya na chama si mazuzu wa kupuuzia au kushindwa kusimamia dhamana na wajibu walionao au kushindwa kuyatolea maelezo na majibu sahihi au yakinifu madai yote yanayoweza kujitokeza .
Kwa bahati mbaya sana utaratibu anaoutaka mtu aliyejiita mwanachama na kada unaweza kufanyika kwenye vyama vingine ambavyo naamini baadhi yake havina Katiba, Kanuni na havifuati miiko ma maadili waliojiwekea katika kufikia utatuzi au kusaka ufumbuzi wa masuala yenye utata .
Tulichokiona katika madai ya mtu huyo aliyejiita mwanachama na kada wa CCM , kwanza tunaweza kumwita ni shabiki maandazi na shawishi wa maandalizi ya kutaka kuzusha vurugu, kuamsha hamkani na tafran aidha ndani ya chama au kwenye jumuiya za chama si vinginevyo
Kama angekuwa ni mwanachama mwenye kufuata misingi ya utii, nidhamu , anayejiheshimu, anayetambua hadhi na heshima ya chama chetu na jumuiya zake, asingekuwa muflis wa kutofuata taratibu halali za kuwasilisha madai yake.
Nasema kwa kupungukiwa kwake ufahamu wabutaratibu na uendeshaji wa kazi za jumuiya yetu ameamua kuwa akipayuka na kusaka umaarufu usioweza kumpatia daraja lolote la heshima mbele ya chama chetu na jumuiya zake.
Ikiwa kweli mtoa shutuma ni mwanachama damu wa CCM, mwana jumuiya halisi aidha ya Wazazi, Wanawake au Vijana, anashindwa nini kuwasilisha madai yake kwa maandishi na vielelezo katika ngazi husika iwapo mkweli, mstaarabu na mpenda uwazi na iwqpo hana sifa ya ulipyoto na umangimeza .
Jumuiya yetu inajua na kushughulikia mambo mengi mazito ambavyo mtoa shutuma huyu aliye kizani , hayajui mwanzo wala mwisho wake na hata akitakiwa aseme au kutaja majina ya anaotuhumu kwa wizi au ufisadi, naamini atapata kigugumizi kwasababu hana analolijua zaidi ya kutumika kama mkanda wa kaseti na kujivika joho la ukuwadi wa kisiasa.
Masuala ya kitaasisi siku zote hushughulikiwa kwa mujibu wa taratibu husika na wala haitokezei kwa Chama au Jumuiya ilio na viongozi makini na waaminifu , wakapita barabarani na kuanza kubwabwaja upuuzi nje ya vikao kama afanyavyo yeye na pengine genge lililo nyuma yake.
Alipayuka kuhusu mashamba ya Igumbiro akiwa hajui chimbuko lake, hana ushahidi, vielelezo wala viambatanisho vya madai yake.
Baada ya kusoma madai yake butu Agosti 12 mwaka huu tuliamua kukaa kimya si kwa kuwa tunamuogopa au kuhofia lolote , tulifanya vile kwasababu wakati ule jumuiya ilikuwa katika vikao vyake muhimu vya kikanuni hivyo isingekuwa vyema kujibishana maswali yasioisaidia jumuiya yetu.
Viongozi na wanachama majasiri, werevu na wenye uthubutu ,siku zote husema au kujenga hoja kwenye vikao halali vya kikatiba na si kutoa madai au matamshi kwenye vilabu vya pombe au majukwaa ya uzandik.
Napenda kutumia hadhira hii kuwahakikishia wana jumuiya wote wa UVCCM kwamba masuala yote yenye kutia shaka, utata na kuleta mkangamyiko , yatashughukikiwa ipasavyo kwa kufuata taratibu husika na kila kwa uchafu utajitenga kama bahari inavyotapika taka na kurudi fukweni.
Kwanza ifahakike kuwa si jambo jepesi na rahisi sana kwa mtu mwenye maarifa na akili timamu afike hatua ya kutoa tuhuma au lawama kuhusu upotevu aidha wa mali, ufujaji fedha au miradi ya jumuiya bila kukusanya ushahidi, vielelezo na viambatanisho halisi vinavyosaidia kuleta maana kamili.
Pili niliwajuza wana habari kuwa uamuzi wa kuanika kila jambo , mashamba ya Igumbiro si mwisho wetu, tutakwenda kila panapotiliwa shaka kwa kufuata taratibu zetu kisha tutaeleza tulioyabaini na kutaja majina ya waliohusika kufuja, kuiba au kuvunja taratibu za kikanuni.
Nchi yetu ni kubwa,ina vijiji, kata, shehia/Tarafa,wikaya na mikoa. Kote huko zipo mail na rasilimali za jumuiya na wala si Igumbiro au Gymkhana na Darajani.
Nilikisema kabla wakati wa ziara zangu katika baadhi ya Mikoa na baada ya kumakizika kikao cha Dodoma wiki ya jana kuwa kila pahala panapotuhusu tutapapekua, tutafanya ukaguzi , tutahakiki mali zote , vitega uchumi na kuipitia mikataba .
Hatuwezi kufanya yote hayo kwa kukurupuka au kwa shijikizo la mtu anayejiita kada na mwanachama .Hata wakati tukipekua sakata la mashamba hakuituma jumuiya, hakuishinikiza na wala huyo aliyejiita kada hakujua kuna lpi limetokea na ushahidi wake ukoje na wa kiwango gani.
Nitumie nafasi adhimu kuwaasa na kuwaonya pia nikiwataka wana jumuiya yetu watambue kuwa hatuwezi kuishi bila kuheshimu au kutofuata utaratibu, UVCCM tuna utaratibu wetu wa kuongoza pia kushughulikia masuala yetu yakiwa mepesi au magumu.
Hakuna usiri, kificho wala hakuna anayehofia au kupania kumkinga mtu yeyote ambaye atakuwa ameehusika kufuja mali, kudumaza miradi au ameshiriki kutenda hujuma yoyote akaachiwa atambe.
Ahsanteni sana kwa kunisililiza.
Shaka Hamdu Shaka (MNEC)
Kaimu Katibu Mkuu UVCCM
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment