Wednesday, 5 July 2017
HALIMA MDEE ATIWA MBARONI NA POLISI
Mbunge wa Kawe, Halima Mdee (Chadema) jana jioni alikamatwa na Jeshi la Polisi akiwa nyumbani kwakeMakongo Juu jijini Dar es Salaam kwa amri ya Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Alli Hapi na kupelekwa katika Kituoni cha Polisi Oysterbay.
Katibu wa CHADEMA jijini Dar, Henry Kilewo amethibitisha kukamatwa kwa Mbunge huyo ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake la CHADEMA (BAWACHA).
“Ni kweli Halima amekamatwa na Polisi na kupelekwa kituoni Oysterbay,“ alisema Kiwelo.
Kamanda wa Polisi, Mkoa wa Kipolisi Kinondoni, Suzan Kaganda amesema amefanya hivyo kwa amri ya mkuu huyo wa wilaya.
“Wapi kakamatwa? Sisi tunachojua ni kuwa tunatekeleza agizo la DC (mkuu wa wilaya) mengine muulize kamishna wa kanda maalum, nimetimiza,” alisema Kaganda.
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Ally Hapi jana aliliagiza Jeshi la Polisi kumkamata na kumweka ndani Mbunge wa Kawe (Chadema), Halima James Mdee kwa madai kuwa kauli yake aliyoitoa juzi, Jumatatu wakati akiongea na wanahabari ni ya uchochezi na ya kumfedhehesha Rais John Magufuli.
Ujumbe wa Halima Mdee baada ya kukamatwa ulisemeka: “Wamekuja polisi kunichukua home! As we speak naelekea kituo cha polisi, probably Oysterbay au Central. Wasaidizi wangu watakuwa na taarifa zaidi za ninakoelekea!”
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment