Na Chibura Makorongo, Itilima
MWENYEKITI wa UDP Taifa, John Cheyo, amewataka Watanzania kuchagua rais bora na makini na kamwe wasiyumbishwe wala kushinikizwa na vyama vya siasa.
Amesema ni muhimu kwa taifa kuongozwa na kiongozi mwadilifu na asiye na doa ili kupata maendeleo ya haraka.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampeni za UDP zilizofanyika katika Kijiji cha Inalo, juzi, Cheyo alisema chake hakina mgombea urais na kuwataka wapiga kura kuchagua mtu mwadilifu na mwenye uwezo wa kuliongoza taifa.
Alisema baadhi ya vyama vya siasa vimeshindwa kufanya siasa, badala yake vinafanya mikutano ya matusi hali inayowafanya wananchi washindwe kuwa na imani na vyama hivyo.
‘’Nchi inaongozwa na rais makini na mwadilifu, mchagueni mtu safi na asiye na doa,” alisema.
Cheyo alisema ametoka mbali katika kuwakomboa watu wa Itilima na kuwataka kutambua kuwa siasa ni sera na kuwatumikia watu.
Naye Kaimu Katibu Mkuu wa UDP, Isack Manjoba, alisema sera ya chama hicho ni ya kutenda haki kwa kila mtu hivyo, vyama viwaache wananchi wafanye uamuzi wenyewe.
No comments:
Post a Comment