Tuesday 8 September 2015

RAIS KIKWETE AWAPA POLE WALIOJERUHIWA MKUTANO WA MAGUFULI MOOGORO

Rais Jakaya Kikwete akiongea na Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya  Mkoa wa Morogoro Dkt. Ritha Lyamuya baada ya kuwajulia hali majeruhi wa msongamano baada ya mkutano wa kampeni uwanja wa Jamhuri Morogoro jana
Mwishoni Rais Kikwete aliongea na wanahabari wa kutoka vyombo mbalimbali na kueleza masikitiko yake kwa yaliyotokea jana Uwanja wa Jamhuri baada ya mkutano wa kampeni kumalizika
Rais Kikwete akitoa mapendekezo ya kupanua hospitali hiyo ambayo ina eneo kubwa lakini majengo machache ya chini. Alipendekeza uongozi wa hospitali na mkoa ubuni namna ya kuipanua kwa kujenga majengo ya ghorofa ili kuwepo na wodi na sehemu nyingi zaidi za huduma
Rais Kikwete alizongwa na wananchi waliokuwa na hamu ya kuongea naye
Rais Kikwete akiongea na wanafunzi waliokuwepo hospitalini hapo kumtembelea mgonjwa
Rais Kikwete akimpa pole mvulana ambaye aligongwa na gari wakati akielekea kumsikiliza mgombea Urais kwa tiketi ya CCM Dkt John Pombe Magufuli katika mkutano wa kampeni Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro jana
Rais Kikwete alitumia wasaa huo kuwapa pole wagonjwa wengine waliokuwa wamelazwa wodi moja na majeruhi hao. Hapa anamfariji mtoto aliyevunjika mguu wakati akicheza kwenye mti
Rais Kikwete na Mama Salma Kikwete wakimpa pole  mmoja wa majeruhi Bi Flora Maduka akiwa kitandani pake hospitalini hapo baad ya kujeruhiwa katika msongamano huo

No comments:

Post a Comment