JUMUIA ya Wazazi CCM
imemtaja mgombea wa Urais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein ni mtu mwenye
uwezo mkubwa kuliko viongozi wote wanaogombea nafasi hiyo visiwani hapa.
Pia imesema ahadi anazotoa
mgombea wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad kuwa akichukua urais ataibadilisha
Zanzibar na kuwa Singapore ni uongo mkubwa.
Naibu Katibu Mkuu wa Wazazi
Zanzibar, Najma Giga, alisema Maalim Seif si mtu makini na anachokizungumza
hakijui ndiyo maana amekuwa mtu wa
kusema kila kitu.
Alisema Maalim Seif ni
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, na ni mtu muhimu kwa Rais Dk. Shein kwa
sababu ana uwezo wa kumfuata au kumpigia simu muda wowote kama ana njia za
kuifanya Zanzibar kuwa Singapore.
"Sasa kama ameshindwa
kumshauri Dk. Shein ili aifanye Zanzibar kuwa Singapore ndani ya miaka mitano
atawezaje kuifanya kwa siku 100. Wazanzibari tusidanganywe na huyu mtu ni mwongo
sana,” alisema.
Alisema Dk. Shein ameweza
kufanya mambo mengi ikiwemo kuhakikisha kuwepo kwa amani ya kudumu na hata
kukifanya Chama Cha Mapinduziv (CCM) kutembea kifua mbele kutokana na
kutekeleza mambo mengi.
Alisema mtu sahihi wa
kuipa Zanzibar maendeleo ni Dk. Shein kwa kuwa ni mmoja wa kiongozi bora na
mwenye maono ya mbali katika kuipa sifa Zanzibar.
Katika hatua nyingine,
Naibu Katibu Mkuu huyo aliwataka waangalizi wa kimataifa wa uchaguzi waliokuja
visiwani hapa.
Alisema litakuwa jambo la
ajabu, endapo waangalizi hao watashindwa kufuata taratibu zilizowekwa na Tume
ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) na badala yake kutenda mambo kinyume na
wanavyotakiwa.
Kwa mujibu wa Naibu Katibu
Mkuu huyo, endapo waangalizi hao watashindwa kufuata taratibu hizo, watashindwa
kuandika ripoti zitakazotokana na uchaguzi huo.
@@@
Watakiwa kupewa elimu ya
mpigakura
WAZANZIBAR wametakiwa
kupewa elimu ya mpigakura na Tume ya
Uchaguzi Zanzibar (ZEC) katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi mkuu.
Pia wananchi walioshindwa
kuchukua shahada zao za kupigia kura wanapaswa kwenda ofisi za ZEC kuchukua
vitambulisho hivyo ili waweze kupiga kura.
Naibu Katibu Mkuu wa
Wazazi, Najma Giga, alisema wananchi wa Pemba na Unguja wanapaswa kushiriki kwa
wingi kwenye uchaguzi huo, kwa kuwa ni haki yao kikatiba.
Alisema tunaiomba ZEC itoe
elimu kwa mpigakura lakini pia sisi jumuia tunawaomba wananchi kuwa katika
karatasi ya mpigakura wakiona picha ya Dk. Ali Mohamed Shein, waweke alama ya
vema.
Naibu Katibu Mkuu huyo,
alisema kila mwananchi anapaswa kujitokeza kwa wingi kwenda kupiga kura ifikapo
Oktoba 25, mwaka huu kwa kuwa ndiyo fursa muhimu ya kuhakikisha Dk. Shein
anaendelea kubakia madarakani.
No comments:
Post a Comment