Saturday, 10 October 2015

KINANA AWACHACHAFYA WAPINZANI KIGOMA

 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwasili kwenye uwanja wa shule ya msingi Katanga,Kasulu mkoani Kigoma tayari kunadi sera za CCM
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akimnadi mgombea ubunge wa jimbo la Kasulu Kusini Ndugu Agustino Zuma Ole kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika viwanja vya shule ya msingi Katanga, Kasulu,mkoani Kigoma.
Mgombea ubunge wa jimbo la Kasulu Kusini Ndugu Agustino Zuma Ole akiomba kura kwa wakazi wa Kasulu Kusini mbele ya Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika kwenye viwanja vya shule ya msingi Katanga.
Mgombea ubunge wa Jimbo la Kasulu mjini Ndugu Daniel Nswanzigwanko akizungumza na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana kabla ya kuhutubia wananchi waliojitokeza kwa wingi kwenye mkutano wa kampeni za CCM uliofanyika kwenye uwanja wa CCM Kasulu
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wananchi waliojitokeza kwa wingi kwenye mkutano wa kampeni za CCM uliofanyika kwenye uwanja wa CCM Kasulu mjini

No comments:

Post a Comment