Saturday, 10 October 2015

CCM YAMTEUA MRITHI WA KOMBANI


KAMATI Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM,  imemteua Goodluck Mlinga kugombea nafasi ya ubunge kwenye jimbo la Ulanga Mashariki.
Mlinga ameteuliwa kugombea nafasi hiyo baada ya kifo cha aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo kwa miaka 10 , ambaye alikuwa akigombea tena, Selina Kombani, kufariki dunia Septemba 24, mwaka huu.
Taarifa iliyotolewa jana na CCM Ofisi Ndogo, Lumumba jijini Dar es Salaam, ilisema uteuzi huo wa Mlinga umekuja baada ya kupata kura 731 kati ya 1,025 ambazo ni sawa na asilimia 71,  kwenye kura za maoni zilizopigwa Oktoba 7, mwaka huu.
Wanachama wengine saba wa CCM, walioshiriki kinyang’anyiro hicho waliridhishwa na namna ambavyo upigaji kura ulivyofanyika kwa kuzingatia misingi ya demokrasia na uwazi.
Wanachama walioshiriki kugombea nafasi hiyo ni Daudi Kitolero, Herieth Mwakifulefule, Pontiano Kiapo, Wencheslous Ikumula na Agustino Matefu.
Wengine ni Thabiti Dokodoko na Azizi Azizi ambao wote wameahidi kumuunga mkono mgombea Mlinga.
Uchaguzi mdogo wa jimbo hilo unatarajiwa kufanyika Novemba 22, mwaka huu.

No comments:

Post a Comment