Na Rashid Zahor
ILIKUWA vigumu kuamini, hasa kutokana na ukweli kwamba Jiji la Dar es Salaam, lina mkusanyiko wa watu wengi na wenye itikadi za vyama tofauti na pia ni ngome ndogo ya baadhi ya vyama vya upinzani, lakini ndivyo hali ilivyokuwa.
Kuanzia saa 2.30 asubuhi, wakazi wa Jiji hilo walianza kujipanga barabarani katika maeneo mbalimbali, ambako msafara wa mgombea urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. John Magufuli ulipita huku wengine wakifika mapema kwenye viwanja, ambako mikutano yake ya hadhara ilifanyika.
Katika maeneo mengi wanachama na wafuasi wa CCM ndio walionekana kujaza mitaa huku wakiwa wamevaa sare za Chama na kushika mabango yenye picha za Dk. Magufuli. Maeneo mengi yalikuwa yamepambwa kwa bendera za CCM, zenye rangi ya kijani na njano.
Dalili za mafuriko ya watu kwenye mikutano hiyo zilianza kujionyesha saa nne asubuhi, wakati alipofanya mkutano wake wa kwanza kati ya mitano, uliofanyika Kigamboni na kuhudhuriwa na maelfu ya wananchi.
Dk. Magufuli, ambaye aliwasili Dar es Salaam, saa 3.30 asubuhi kwa ndege, akitokea Mwanza, pia alifanya mikutano mingine katika majimbo ya Mbagala, Temeke, Ubungo na Kinondoni. Pia alifanya mikutano midogo mitatu kutokana na kuzuiwa barabarani.
Katika mikutano hiyo, ambayo Dk. Magufuli alitumia zaidi ya saa tano kuwahutubia wananchi, alisema ameshaanza kusikia harufu ya urais kutokana na mikutano yake kufurika mamia ya wananchi na kuahidi kumpigia kura nyingi.
Aidha, Dk. Magufuli aliwataka wananchi wasiwachague viongozi wenye maamuzi magumu, badala yake wachague viongozi makini, katika uchaguzi mkuu wa rais, wabunge na madiwani, unaotarajiwa kufanyika Jumapili kote nchini.
Mgombea huyo pia aliwaeleza wananchi hao kuwa, Tanzania inahitaji kuwa na rais mkali ili mambo yaweze kwenda mbele, vinginevyo nchi itakwama.
Pia aliapa kumshughulikia kigogo mmoja wa serikali, aliyekwamisha kukamilika kwa mradi mkubwa wa maji katika Jiji la Dar es Salaam, kutokana na kuifungulia kesi serikali mahakamani ya kupinga nyumba yake kubomolewa ili kupisha mradi huo.
KIGAMBONI KUCHELE
Akihutubia mkutano wake wa kwanza uliofanyika Kigamboni, kuanzia saa 4.07 hadi saa 4.57, asubuhi, Dk. Magufuli aliwaahidi wananchi kuwa, atakapokuwa rais, ataruhusu Daraja la Kigamboni kutumika bure kwa wanaotembea kwa miguu.
Aidha, mgombea huyo aliahidi kuupa mji wa Kigamboni hadhi ya kuwa wilaya ili uweze kuwa na maendeleo makubwa zaidi kutokana na mipango inayofanywa na serikali ya kuufanya mji huo uwe mpya.
"Kigamboni inastahili kuwa wilaya, nitakapokuwa rais, nitalishughulikia suala hilo, sitawaangusha, nitawabeba,"alisema Dk. Magufuli huku akishangiliwa kwa mayowe mengi na wananchi.
Kutokana na mabadiliko yanayotaka kufanywa na serikali katika mji huo, Dk. Magufuli aliahidi kuwa serikali yake itajenga hospitali kubwa na yenye hadhi ya wilaya, ambayo itakuwa na huduma na vifaa vyote muhimu vya tiba.
Dk. Magufuli alisisitiza kuwa siku zote maamuzi yake ni makini kwa sababu lengo lake kubwa ni kuwaendeleza Watanzania, hasa waliomasikini ili waondokane na hali hiyo.
Msafara wa mgombea huyo ulipokewa kwa furaha kubwa katika maeneo yote ya Kigamboni, ambako umati wa wananchi ulilipuka mayowe ya kumshangilia na kuimba 'rais, rais, rais.'
Kutokana na kufurahishwa na mapokezi hayo, Dk. Magufuli alisema anataka kushinda uchaguzi wa mwaka huu wa kishindo kwa kupata asilimia 99 na asilimia moja iliyobaki wagawane wapinzani.
Aidha, alisema mapokezi hayo yamemfanya aanze kusikia harufu ya urais, lakini aliwataka wananchi wasianze kushangilia, badala yake wajitokeze kwa wingi siku ya uchaguzi kwenda kupiga kura.
Akihutubia mkutano uliofanyika Zakhem, Mbagala, mchana, mgombea huyo alisema mabadiliko ya kweli yanapatikana kwa kufanyakazi na kuwaletea maendeleo wananchi kwa kuwapelekea huduma za maji, umeme na afya ili kuboresha maisha yao.
Aliwatahadharisha wananchi hao waepuke kuwachagua viongozi wenye maamuzi magumu kwa sababu yanaweza kusababisha madhara mbalimbali kwa jamii. Badala yake aliwataka kuchagua viongozi wenye maamuzi makini.
Wakati msafara wake ukiondoka Mbagala kwenda Temeke, baadhi ya wananchi waliusindikiza kwa maandamano huku wakiimba 'rais, rais, rais'.
Akihutubia mkutano uliofanyika kwenye viwanja vya Mwembe Yanga, Temeke, mgombea huyo alisema Tanzania inahitaji kuwa na rais mkali ili mambo yaende mbele.
Alisema iwapo rais atakuwa mpole na kuwaacha watendaji kufanya wanavyotaka, itakuwa ndoto kwa nchi kupata maendeleo.
Kivutio kikubwa kwa mgombea huyo wakati akiwa katika Jiji la Dar es Salaam, kilikuwa wakati aliposimamisha msafara wake eneo la mataa ubungo, na kuwasalimia wafuasi wa CHADEMA na CCM, waliokuwa wamejipanga barabarani.
Wakati akizungumza na wananchi hao, baadhi ya wafuasi wa CHADEMA walikuwa wakitamka maneno 'peoples power', lakini walizidiwa nguvu na wenzao wa CCM waliokuwa wakiimba 'rais, rais, rais.'Wafuasi hao waliusindikiza msafara wa Dk. Magufuli hadi eneo la darajani.
Msafara wa Dk. Magufuli pia ulisimama katika maeneo ya Shekilanga na Sinza Kijiweni, ambako mamia ya wananchi walijipanga barabarani, wakiwa na kiu ya kumuona na kumsikiliza. Muda wote alipokuwa akiwahutubia, wananchi hao walikuwa wakiimba 'rais, rais, rais.'
Fungakazi ilikuwa pale mgombea huyo alipowasili kwenye uwanja wa TP, Sinza, Dar es Salaam, ambako alipokelewa kwa shamrashamra nyingi na kuwahutubia wananchi wa jimbo la Ubungo.
Katika mkutano huo ulioanza saa 8.24 mchana, Magafuli aliwaeleza wananchi kuwa amefurahishwa na mapokezi aliyoyapata, ikiwa ni pamoja na kuwapongeza viongozi wa CHADEMA na CUF kwa kuupamba mji kwa bendera za vyama vyao, ikiwa ni ishara ya kumpokea na kumkubali.
Alisema mapambo hayo yamedhihirisha wazi kuwa vyama hivyo viwili, ambavyo ni miongoni mwa vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA), vinamkubali na kutambua kuwa ndiye rais ajaye wa awamu ya tano ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Dk. Magufuli alihitimisha mikutano yake juzi kwa kufanya mkutano mkubwa wa hadhara kwenye viwanja vya Biafra, Jimbo la Kinondoni, wilaya ya Kinondoni, ambao ulihudhuriwa na maelfu ya wananchi.
Akihutubia mkutano huo, Dk. Magufuli alisema anakerwa na kitendo cha kigogo mmoja wa serikali, kufungua kesi mahakamani kupinga amri ya kuibomoa nyumba yake ili kuwezesha mradi mkubwa wa maji katika Jiji la Dar es Salaam.
Alisema kitendo cha kigogo huyo kufungua kesi mahakamani na mahakama kuchelewa kutoa uamuzi, kimesababisha wakazi wa Jiji la Dar es Salaam, wakose huduma ya maji safi na salama, huku wengine wakifa kutokana na ugonjwa wa kipindupindu.
"Yupo tajiri mmoja amejenga nyumba yake juu ya mabomba, alipoambiwa aibomoe, aliipeleka serikali mahakamani, kesi hadi leo inaendelea, haijulikani lini itatolewa uamuzi na wananchi wanaendelea kupata shida.
"Watu wanakufa kwa kipindupindu, wanakosa maji safi, wao wanakunywa maji safi. Hivi watu hawa watakwenda kusema nini kwa Mungu.
"Ningekuwa mimi waziri wa maji, ningeibomoa ile nyumba kisha niende kufungwa kwa ajili ya kuwatetea wananchi wangu. Hata hivyo, zimebaki siku tano kabla sijawa raisi. Watu wanasema mimi mkorofi, lakini mimi si mkorofi, wakorofi ni waliofungua kesi na wanaochelewa kutoa uamuzi,"alisema.
Alisema iwapo mradi huo ungekuwa umeshaanza, Jiji la Dar es Salaam, lingekuwa linapata lita milioni 700 za maji kwa siku, ambazo zingeweza kuwahudumia wakazi wote wa Jiji na kumaliza kabisa tatizo la maji.
Dk. Magufuli alisema atakapokuwa rais, hataruhusu mambo kama hayo na kwamba, akiwa waziri wa ujenzi, amewahi kuwatimua wakandarasi 3,230 na wafanyakazi 400 wa mizani kwa makosa ya kupokea rushwa.
"Ndio maana nasema nipeni urais. Mniamini, nikafanyekazi, msiseme nimeshapata urais, nendeni mkanipigie kura,"alisema Dk. Magufuli.
Mgombea huyo pia alizungumzia tatizo la kukatika mara kwa mara nchini, ambalo alieleza wazi kuwa linatokana na hujuma za wazi zinazofanywa na vigogo wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), kwa kufungulia maji kwenye mabwawa ya umeme ili wapate tenda ya kununua mafuta.
"Nikiwa rais, umeme utapatikana kwa uhakika, najua hii ni hujuma ya ajabu, watu wanafungulia maji makusudi. Najua vitu vingi sana katika nchi hii, ndio maana nataka mnipe urais ili niwashughulikie watu hawa,"alisema huku akionekana dhahiri kukerwa na vitendo hivyo.

No comments:
Post a Comment