Na Mwamvua Mwinyi ,Kibiti
MAUAJI mengine yatokea wilaya ya Kibiti mkoani Pwani ,ambapo inadaiwa mtendaji wa kijiji cha Mangwi,Shamte Rashid Makawa na mwenyekiti wa kijiji cha Mangwi ,kata ya Mchukwi ,Hamis Mkima wameuawa kwa kipigwa risasi na watu wasiojulikana.
Aidha watu hao baada ya kumuua Shamte walichoma moto nyumba yake na kuteketeza mali zote .
Mbali ya hayo ,mwenyekiti wa kitongoji cha Londo aliyejulikana kwa jina moja la Michael Nicholas amejeruhiwa kwa kutobolewa macho ,na inadaiwa hali yake ni mbaya .
Akizungumzia matukio hayo ,katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kata ya Mchukwi ,Saidi Hassan Seta,alisema tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia jana .
Alieleza kwamba ,Shamte akiwa amejipumzisha na familia yake nyumbani kwake ,majira ya saa tatu usiku ,walishtukia watu wanaingia sebuleni na kumpiga risasi peke yake .
Seta alisema ,walimtoa marehemu nje ya nyumba na familia hiyo ,kisha kuchoma moto nyumba na kuteketea mali zote .
Hata hivyo mwenyekiti wa kitongoji cha Londo ,Michael ,alikimbizwa katika hospital ya mission ya Mchukwi kwa matibabu zaidi .
Nae kamanda wa polisi mkoani Pwani ,Onesmo Lyanga ,alisema bado wanafuatilia matukio hayo .
Alieleza wanaendelea kuwasaka watu wanaojihusisha na mtandao huo unaoteketeza roho za wasio na hatia .
Mkuu wa mkoa wa Pwani ,Mhandisi Evarist Ndikilo ,kila wakati amekuwa akisisitiza jamii kuwafichua wale wanaowadhania ni wahusika wa matukio hayo .
Akitoa maoni yake ,mwenyekiti wa jumuiya ya vijana (UVCCM)mkoani Pwani ,Mohammed Nyundo ,alieleza wauaji hao inaonekana hawapo porini.
“Tunaishi nao Mjini, na ndio maana wapo updated, viongozi wetu wanapokutana na kuongea na Jamii wao wanapata taarifa kwa muda muafaka, wanafanya matukio agaist. Pia wana mawasiliano ya mara kwa mara. “
“Na nia yao kubwa ni kutaka kuchokonoa mamlaka ili zichukue hatua ili wao wakae pembeni na serikali iendelee kushughulika na suala hili na kuacha mingine. Hofu yangu hili jambo lisije kuwa ni Agenda ya Muda mrefu hadi kufikia 2020. ” anaendelea Nyundo.
“;Kuna haja ya kuwa na Collective efforts za jambo hili kati ya viongozi wenyeji na mamlaka za kidola. Pia approach ya viongozi wa kijeshi kwenda kuzungumza na wazee katika eneo la tukio nadhani si sahihi kwa mazingira ya rufiji.” alisisitiza Nyundo.
Alisema baadhi ya wazee na viongozi wa huko Ikiwezekana waitwe na mazungumzo yafanyike .
Nyundo aliiomba jamii kuacha kutumia mitandao vibaya kwa kuchora ama kukebehi na kuohanisha na matukio ya Kibiti na Rufiji kwani kwa kufanya hivyo ni kuchochea ama kuwaumiza wale wanaoguswa na matukio yanayoendelea .
Mwenyekiti huyo wa UVCCM Pwani ,alibainisha kwamba ,masuala ya Kibiti yanaumiza na wakati vyombo vya dola vikiendelea na mapambano basi jamii isitumie Kibiti kwenye vikatuni na mitandao .kwa ubaya .
Kwa upande wa wakazi wa Mangwi ,akiwemo Ally Jumanne na Rehema Shafii ,walisema imefikia hatua ya kuona ni matukio ya kawaida lakini bado wanaishi kwa hofu .
“Tusipo kua makini sumu hii itaingia na wilaya nyingine za mkoa wa Pwani. Tuelekeze akili zetu hapo Ili kulithibiti hili mapema” alisema Ally .
Rehema ,aliviomba vyombo vya dola vitafiti kiini cha masuala ya kisiasa kwani kuuawa askari polisi haimaanishi kuondoa fikra za kiitikadi .
“Tatizo hapa ni tangu upande wa pili kuangukia pua uchaguzi uliopita wa serikali za mitaa (2015) ambapo CCM ilishinda vitongoji na vijiji vingi .Lengo kuu ni kuishinda CCM 2019 ” aliainisha Rehema .
Aliomba jeshi la polisi na wasiri wake waongeze kasi ya kuendana na mbinu wanazotumia wauaji hao ili kuwakamata na kujua chanzo na kiini cha matukio hayo .
Mnamo june 21 mwaka huu, askari polisi wawili wa kikosi cha usalama wa barabarani ,wilayani Kibiti waliuawa kwa kupigwa risasi ,katika kijiji cha Msafiri,Kata ya Bungu wakiwa kazini.
Mbali na hayo pia gari moja na pikipiki za askari hao ,zilichomwa moto .
Ndani ya mwezi mmoja watu wanne wameuawa Kibiti na Rufiji ,wawili waliokotwa wakiwa wamekufa ,mmoja amenusurika kifo kwa kupigwa risasi ya kichwa .
Huku matukio haya yakidaiwa kuanza mwaka 2015 na hadi sasa wanaosadikiwa kuuawa ni 37 kati yao askari Polisi ni 13 .

No comments:
Post a Comment