Wednesday, 28 October 2015

MAGUFULI ANUSA IKULU





Na Mwandishi Wetu
MGOMBEA Urais wa CCM, Dk. John Magufuli, anaelekea kushinda katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu, baada ya kupata ushindi katika maeneo mengi ambayo matokeo yake tayari yametangazwa hadi kufikia jana.
Kwa mujibu wa matokeo ya urais yaliyotangazwa jana usiku na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Dk. Magufuli ameshajikusanyia kura zaidi ya milioni 1.7 huku mpinzani wake, Edward Lowassa akijikongoja kwa kura milioni 1.2.
Idadi hiyo ya kura ni sawa na asilimia 56 kwa Magufuli na asilimia 41 kwa Lowassa kutokana na kura zilizokwisha kuhesabiwa mpaka sasa.
Leo, NEC inatarajiwa kuendelea kutangaza sehemu kubwa ya matokeo ya urais wa Tanzania kwa kuwa awali ilipanga kumtangaza mshindi ifikapo Oktoba 29, mwaka huu (kesho).
Sehemu kubwa ya matokeo yaliyotangazwa hadi jana ni ya majimbo ya uchaguzi ambako CCM imepata viti vingi kuliko wapinzani wao wakuu, CHADEMA, wanaoungwa mkono na kundi la UKAWA.
Kwa kawaida, chama kinachopata viti vingi bungeni ndiyo pia hushinda katika uchaguzi mkuu hivyo, ushindi wa majimbo unaonyesha ishara nzuri kwa Dk. Magufuli na CCM.
Hadi jana jioni, CCM ilikuwa  imepata majimbo 123 kulinganisha na majimbo 32 ya CHADEMA, huku CUF ikiwa imevuna majimbo 22 kufikia jana jioni wakati tukienda mitamboni.
Taarifa za awali kutoka mikoa yenye wapigakura wengi zinaonyesha kuwa, Dk. Magufuli anaongoza kwa kiasi kikubwa na uwezekano wa kushindwa katika maeneo hayo ni finyu.
Mikoa inayoongoza kwa wapiga kura wengi nchini ni Dar es Salaam, Mbeya, Mwanza, Morogoro, Kagera, Tanga na Tabora na Magufuli; kwa mujibu wa taarifa hizo za NEC anaongoza hadi sasa.

Majimbo ya ubunge kwa CCM
Tanga
Katika mkoa huu wenye majimbo 12, CCM ilikuwa na uhakika wa ushindi katika majimbo 10 huku moja la Tanga Mjini likichukuliwa na Chama cha CUF.
Majimbo ambayo CCM imepata ushindi ni Handeni, Muheza, Korogwe Mjini, Korogwe Vijijini, Bumbuli, Pangani, Mkinga na Mlalo.
Mwanza
Katika mkoa huu muhimu katika Kanda ya Ziwa, CCM inaelekea kupata ushindi katika majimbo ya Nyamagana, Ilemela, Buchosa, Magu, Kwimba, Sumve, Sengerema na Misungwi. Chadema walikuwa na uhakika wa kupata ushindi katika jimbo la Ukerewe pekee.
Dar es Salaam
Hadi jana jioni, CCM ilikuwa imepata ushindi katika majimbo ya Ilala na Segerea huku Chadema ikipata ushindi katika majimbo ya Ukonga, Kawe na Ubungo.
Mbeya 
Katika mkoa huu, CCM imeshinda katika majimbo ya Ileje, Busokelo, Mbeya Vijijini, Rungwe na Mbarali huku ikipoteza katika majimbo ya Mbeya Mjini na Tunduma.
Morogoro
CCM imeshindwa katika majimbo ya Mikumi, Mlimba na Kilombero, lakini imepata ushindi katika majimbo ya Morogoro Mjini, Morogoro Kusini Mashariki, Ulanga Magharibi, Mvomero na Kilosa.
Tabora
Hadi tunakwenda mitamboni, CCM ilikuwa imeshinda katika majimbo yote 12 ya mkoa huo. Majimbo hayo ni Tabora Mjini, Igalula, Nzega Mjini, Nzega Vijijini, Bukene, Igunga, Urambo, Ulyankulu, Tabora Kaskazini, Kaliua na Tabora Kaskazini.
Kagera
Katika majimbo tisa ya mkoa wa Kagera, CCM imepoteza jimbo moja la Bukoba Mjini, lakini imepata majimbo mengine nane. Majimbo hayo ni Nkenge, Muleba Kusini, Muleba Kaskazini, Kyerwa, Karagwe, Bukoba Vijijini na Biharamulo.
Hadi jioni, mkoa pekee ambao CCM ilikuwa imeshindwa ni Kilimanjaro  ambao hata hivyo, hauko katika orodha ya mikoa yenye wapiga kura wengi.
Hata hivyo, kushindwa kwa CCM Kilimanjaro kunafutwa machozi na ushindi ilioupata katika mikoa mingine, kwa mfano Dodoma, ambako imechukua majimbo yote 10 huku wapinzani wakiambulia patupu.
Kuna mikoa mingine midogo ambayo CCM imeshinda kwa kishindo kama vile Simiyu, Geita, Shinyanga, Katavi, Rukwa na Kigoma.
Kwa sababu hii, UHURU linaweza kubashiri kwamba, Dk. Magufuli ataibuka na ushindi wa kishindo baada ya NEC kutangaza matokeo yote.


MATOKEO YA URAIS
Jimbo la Mkwajuni
CCM-4,686
CHADEMA-3,314
ACT-26

Jimbi la Momba
CCM-28,978
CHADEMA-24,418
ACT-406

JIMBO LA MONDULI
CCM-11,355
CHADEMA-49,675
ACT-107

JIMBO LA MPENDAE
CCM -4,192
CHADEMA-4,048
ACT-14

JIMBO LA MWANGA
CCM-25,738
CHADEMA-15,148
ACT-150

JIMBO LA NEWALA MJINI
CCM-21,269
CHADEMA16,980
ACT-202

JIMBO LA NAMTUMBO
CCM-44,061
CHADEMA-23,036
ACT-566

JIMBO LA NEWALA VIJIJINI
CCM-29,799
CHADEMA-13,958
ACT-412

JIMBO LA RUANGWA
CCM-34,516
CHADEMA-26,827
ACT-319

JIMBO LA SIHA
CCM-18,252
CHADEMA-22,572
ACT-155

JIMBO LA SOLWA
CCM-66,096
CHADEMA-23,510
ACT-645

JIMBO LA TANDAHIMBA
CCM-49,098
CHADEMA-46,288
ACT-803

JIMBO LA TUMBATU
 CCM-5,720
CHADEMA-3,967
ACT-21

JIMBO LA IGALULA
CCM-28,747
CHADEMA-8,593
ACT-342

JIMBO LA ULANGA
CCM-32,297
CHADEMA-20,489
ACT-222

JIMBO LA WAWI
CCM-1,748
CHADEMA-5,216
ACT-19

JIMBO LA ZIWANI
CCM-592
CHADEMA-6,067
ACT-17

JIMBO LA OLE
CCM-681
CHADEMA-5,251
ACT-10

JIMBO LA KUSINI UNGUJA
CCM-5,592
CHADEMA-1,019
ACT-5

JIMBO LA TABORA KASKAZINI
CCM-38,050
CHADEMA-12,410
ACT-508

JIMBO LA MALINDI
CCM-2,581
CHADEMA-5,662
ACT-20

JIMBO LA JANG’OMBE
CCM-6,567
CHADEMA-2,839
ACT-20

JIMBO LA MUHAMBWE
CCM-37,746
CHADEMA-22,804
ACT-1,302

 Jimbo la Chalinze
ACT- 450,
CCM-52,212
 CHADEMA 21,380

 Jimbo la Chonga
ACT- 22,
CCM-1,740
 CHADEMA 3,800

 Jimbo la Chumbuni
ACT- 31
CCM- 5,096
CHADEMA -4,450

Jimbo la Ileje
ACT- 51,
CCM- 26,368
 CHADEMA- 15,651

Jimbo la Kilindi
ACT-324,
 CCM-33,942
 CHADEMA- 12,123

Jimbo la Korogwe Mjini
ACT- 151,
CCM-17,168
 CHADEMA- 9,034

Jimbo la Kwahani
ACT-14,
CCM-6,245
 CHADEMA- 2,689

Jimbo la Lupembe
ACT-259,
CCM-23,061
 CHADEMA 7,466

Jimbo la Madala
ACT-134,
CCM-13,949
 CHADEMA- 4,735

Jimbo la Masasi Mjini
ACT-266,
CCM-24,637
 CHADEMA- 16,778

Jimbo la Mbeya Vijijini
ACT-672,
CCM-24,637
CHADEMA -16,778

Jimbo la Mbeya Vijiji
CCM-62,662
CHADEMA- 47,038
ACT-672


Jimbo la Nungwi
CCM- 4,135
CHADEMA-4,853
ACT-47

Jimbo la Chwaka
CCM- 6,537
CHADEMA- 1,864
ACT – 28

Jimbo la Mtama
CCM- 29,625
CHADEMA- 20,841
ACT-458

Jimbo la Tungu
CCM-8,519
CHADEMA-2,923
ACT-18

Jimbo la Biharamulo
CCM-44, 943
CHADEMA-28,576
ACT-605

Jimbo la Arusha Mjini
CCM-65,107
CHADEMA-15,786
ACT-464

Jimbo la Kibaha Vijijini
CCM-20,805
CHADEMA-11,344
ACT-121

Jimbo la Mwanakwerekwe
CCM-4,206
CHADEMA-4,606
ACT-12

Jimbo la Nachingwea
CCM-46,485
CHADEMA-30,252
ACT-461

Jimbo la Mafia
CCM-11, 153
CHADEMA-9,363
ACT-146

Jimbo la Mkuranga
CCM-45,710
CHADEMA-36,478
ACT-899

Jimbo la Welezo
CCM-2, 615
CHADEMA-2, 582
ACT-10

Jimbo la Magomeni
CCM-5,716
CHADEMA-3,711
ACT-10

JIMBO LA SHAURIMOYO
CCM-5,849
CHADEMA-3,731
ACT-32

JIMBO LA FUONI
CCM-956
CHADEMA-420
ACT-3

JIMBO LA KIKWAJUNI
CCM-6,317
CHADEMA-3,669
ACT-13

JIMBO LA MPANDA VIJIJINI
CCM-37,321
CHADEMA-12,791
ACT-696

JIMBO LA MCHINGA
CCM-13,948
CHADEMA-12,936
ACT-203

JIMBO LA MWERA
CCM-6,430
CHADEMA-5,865
ACT-19

JIMBO LA BUMBWINI
CCM-2,503
CHADEMA-2,822
ACT-11

JIMBO LA UZINI
CCM-6,537
CHADEMA-1,864
ACT-28

JIMBO LA NKASI KASKAZINI
CCM-25,837
CHADEMA-19,891
ACT-216

JIMBO LA CHAKECHAKE
CCM-1,253
CHADEMA-8,779
ACT-15

JIMBO LA NKASI  KUSINI
CCM-21,572
CHADEMA-13,550
ACT-246

JIMBO LA NKENGE
CCM-42,568
CHADEMA-25,840
ACT-307

JIMBO LA AMANI
CCM-4,322
CHADEMA-3,157
ACT-18

No comments:

Post a Comment