Na
Ahmed Makongo, Bunda
MGOMBEA
ubunge katika jimbo la Mwibara, kupitia tiketi ya CCM, Kangi Lugola, maarufu
Kangi Bomba Nati ya Kirumi, ametetea nafasi yake baada ya kumshinda mgombea wa
CHADEMA, aliyewahi kumshinda tena katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2010.
Msimamizi
wa Uchaguzi katika Wilaya ya Bunda, Lucy Msoffe, alimtangaza jana Lugola kuwa
mshindi kwa kupata kura 33,845 na kumshinda Chiriko Haruni wa CHADEMA aliyepata
kura 6,675.
Msimamizi
huyo wa uchaguzi katika jimbo la Mwibara, pia alimtangaza mgombea mwingine kuwa
ni Mtamwega Mgaywa wa ACT-Wazalendo aliyepata kura 521.
Hata
hivyo, mgombea huyo alisikika akisema kuwa alikuwa amejiondoa katika
kinyang’anyiro hicho, licha ya wananchi kumpigia kura bila ya yeye kuwepo wala
kufanya kampeni.
Akizungumza
na waandishi wa habari baada ya matokeo hayo kutangazwa, Lugola alisema kuwa
aliamini kuwa ataibuka na ushindi mkubwa kwa sababu ya utendaji kazi wake
mzuri.
Alisema
kuwa atawatumikia wananchi wa jimbo hilo kama kawaida yake, maana anautambua
mchango wao wa kumwamini tena kuendelea kuwa kiongozi wao katika uchaguzi wa
mwaka huu uliokuwa na ushindani mkubwa.
Aidha,
alisema atapigania jimbo la Mwibara kuwa na halmashauri na wilaya yake ili
kusogeza huduma za kijamii kwa wananchi.
“Madiwani
wa huku juu wakae mkao wa kujitathmini maana tunataka Mwibara nayo iwe
halmashauri na wilaya.
“Tena
mimi nitamsaidia mgombea wetu wa urais ambaye nina amini atashinda urais, Dk.
John Magufuli, kwa kuwatumikia wananchi wetu maana wametuamini na
nitaziendeleza miradi ya maendeleo ambayo tunaendelea kuitekeleza jimboni kwetu,”
alisema.
Katika
jimbo la Bunda Vijijini, mgombea ubunge wa CCM, Boniphace Mwita Getere,
alitangazwa mshindi baada ya kupata kura 12,589 na kumshinda Suleiman Daud wa
CHADEMA aliyepata kura 7,547.
No comments:
Post a Comment