Saturday, 17 October 2015

MKAPA AMNADI MAGUFULI TANGA



NA SOPHIA WAKATI, TANGA

Rais mstaafu Benjamini Mkapa amesema ameamua kuzunguka nchini kuwashawishi Watanzania kumchagua Dk. John Magufuli kuwa Rais kwa sababu CCM ina uzoefu mkubwa wa kuongoza.

Amesema CCM inasifika hata kimataifa kwa kuongoza kwa uadilifu na kufuata maadili tofauti na UKAWA ambayo haina hata sera.

Alitoa kauli hiyo jana wakati wa mkutano wa kampeni wa kumnadi Dk. Magufuli, wabunge na madiwani wa CCM, uliofanyika uwanja wa Tangamano, jijini hapa.

Alisema CCM ni chama kinachopigiwa mfano wa  si kuiongoza Tanzania pekee bali hata ukombozi wa nchi za kusini mwa Afrika ambazo hadi sasa zinajitawala kutokana na kukombolewa na CCM.

Aidha alisema kama leo baadji ya watu wanapanda kwenye majukwaa na kudiriki kusema CCM haijafanya kitu, wanapaswa kupuuzwa kwa kuwa wamekosa ya kusema.

Mkapa alisema watu hao hawafai kupewa kura kutokana na mgombea urais wa UKAWA, Edward Lowassa na Frederick Sumaye anayemnadi, wote walikuwa mawaziri wakuu ndani ya serikali.

“Ndugu zangu sasa leo kama wanadiriki kusema CCM haikufanya kitu, wanyimeni kura Oktoba 25. Msiwachague wataongoza kwa kutumia ilani gani?” alisema Mkapa.
Mkapa  yuko mkoani Tanga kwa lengo la kuwaombea kura wagombea kupitia CCM ili
wananchi wawachague na kuendelea kuongoza nchi.

No comments:

Post a Comment