Monday 5 October 2015

RAIS KIKWETE ATUMA SALAMU ZA RAMBIRAMBI KIFO CHA MCHUNGAJI MTIKILA



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya MrishoKikwete ametuma salamu za rambirambi na maombolezo kumlilia Mwenyekiti waChama cha Siasa cha Democratic Party (DP), Mchungaji Christopher Mtikila, ambayealipoteza maisha katika ajali ya gari iliyotokea alfajiri ya leo, Jumapili, Oktoba 4, 2015,katika Kijiji cha Msolwa, Wilaya ya Bagamoyo, Mkoa wa Pwani.Katika salamu zake za rambirambi kwa Chama cha DP, Rais Kikwete amesema:
“ Nimepokea kwa huzuni kubwa taarifa za kifo cha Mwenyekiti wenu na Mtanzaniamwenzetu, Mchungaji Christoher Mtikila ambaye nimeambiwa amepoteza maishakatika ajali ya gari Mkoani Pwani akiwa njiani kurejea mjini Dar es Salaam akitokeakwao Njombe.”“Kwa hakika, kifo cha Mchungaji Mtikila ni pigo kubwa kwa Chama chaDemocratic Party ambacho kimempoteza kiongozi wake mkuu. Aidha, kifo hicho ni pigo kwa medani za siasa katika Tanzania na kimetunyang’anya mmoja wa viongozihodari na wazalendo, aliyekuwa na msimamo thabiti na usioyumba katika kuteteamambo ambayo aliyaamini katika maisha yake yote,” amesema Rais Kikwete nakuongeza:
“Ni jambo la kusikitisha pia kuwa tunampoteza Mchungaji Mtikila katikakipindi cha mchakato muhimu wa kisiasa nchini ambako mchango wake ulikuwaunahitajika sana. Hakika, tutamkosa mwenzetu katika uwanja wa siasa za nchiyetu.”

Ameendelea Rais Kikwete,
“Nawatumieni nyie wana-democratic Party salamuza dhati ya moyo wangu na pole nyingi kwa kuondokewa na kiongozi wetu mkuu, wamiaka mingi na wenye uzoefu wa uongozi wa chama cha siasa.”“Aidha kupitia kwenu, napenda kuitumia pole zangu nyingi familia ya Mchungaji Mtikila. Nawapa pole sana wanafamilia, ndugu na maraļ¬ki na napendawajue kuwa niko nao katika kipindi hiki cha majonzi ya kuondokewa na mhimili wa familia. Naungana nao katika majonzi. Aidha, naungana nao katika kumwomba Mwenyezi Mungu, Mwingi wa Rehema, aiweke pema roho ya Mchungaji Christopher Mtikila.

No comments:

Post a Comment