Wednesday 7 October 2015

WASANII WA KUNDI LA NIMESTUKA WAWATAKA VIJANA KUICHAGUA CCM

Msanii wa bongo movie, Ndende akmwaga sera kwa vijana wilayani Kishapu mkoani Shinyanga
Msanii wa bongo fleva, Inspekta Haroun akimwaga sera kwa vijana kwa njia ya mashairi ya nyimbo
Msanii wa bongo movie, Kajala Masanja akiwasihi vijana kuichagua CCM. Hii ni kampeni ya kijiji kwa kijiji
Yule mchekeshaji Kitale naye yumo. Hapa akiwaeleza vijana umuhimu wa kuichagua CCM
Mrembo wa Tanzania wa mwaka 2014/15, Lilian Kamazima akitumia urembo wake kuwahamasisha vijana kuipigia kura CCM
Mchekeshaji wa filamu, Mboto akitumia fani yake kuwataka vijana waichague CCM
Msanii wa bongo fleva, Ndende akimwaga sera za CCM kwa vijana wenzake

Vijana wakijipanga kwa ajili ya kumsajilimia msanii nyota wa filamu nchini, Ray Kigosi
Skyner Ally naye alikuwepo
 Na Mwandishi Wetu
Msanii Nguli wa filamu nchini, Ray Kigosi, amewaambia watanzania leokuwa makini na kusikiliza sera na kuachana na mihemko ya kisiasa itakayopelekea wao kufanya maamuzi watakayoyajutia baadae.
Kigosi ameyasema hayo alipokuwa katika moja ya mikutano inayoendeshwa na kundi la wasanii lenye kauli mbiu ya Nimestuka, katika jimbo la Kishapu mkoani Shinyanga, ikiwa ni sehemu ya ziara ya kundi hilo inayopita kijiji kwa kijiji katika kuhakikisha kwamba wanawaelimisha vijana wenzao kuhusiana na usikilizwaji wa sera na mapokeo ya demokrasia kwa jamii.
Awali, akiongea kabla ya kuwakaribisha wenzake 12 alioandamana nao, Kigosi amesema yeye alipokuwa Ukawa alikuwa akishuhudia vijana wakihamasishwa kupinga hata mambo yanayoonekana kuwa na tija yaliyofanywa na seriikali jambo ambalo yeye mwenyewe aliliona kuwa ni upotoshwaji wa wazi wazi.
"Naamini kuwa mpinzani, sio kupinga kila kitu, walipaswa pia kutufundisha jinsi ya kukabiliana na maisha kama vijana, lakini nikaja kugundua nimekosea sana kuacha kuungana mkono na Magufuli", alikiri Kigosi.

No comments:

Post a Comment