NA MWANDISHI WETU
WAKATI Watanzania wakijitokeza kwa wingi kwenye vituo vya kupigia kura kufanya uamuzi wa mahali wanataka Tanzania ijayo iwe, mgombea urais kupitia CCM, Dk. John Magufuli, amepiga kura katika kituo cha Shule ya Msingi ya Magufuli na kusema mvua kunyesha ni dalili nzuri na ishara ya ushindi.
Dk. Magufuli ali?ka kituoni hapo saa nne asubuhi, ambapo wakati akipiga kura kuliwa na manyunyu manyunyu ya mvua.
“Mvua kudondoka nahisi ni dalili nzuri,” alisema Dk. Magufuli na kutoa wito kwa Watanzania wa vyama vyote kupiga kura kuwachagua viongozi watakaowaongoza kwa miaka mitano.
Dk. Magufuli aliyasema hayo alipozungumza na waandishi wa habari baada ya kutimiza haki yake ya kupiga kura kwa kumchagua rais, wabunge, wawakilishi na madiwani.
Ilipotimu saa 4.35 asubuhi, baada ya ku?ka kituo namba moja, Dk. Magufuli alienda katika chumba cha kupigia kura ambapo alikabidhiwa karatasi tatu za kuwapigia kura viongozi hao.
Baada ya kuwachagua Dk. Magufuli alionekana akikunja karatasi zake na kisha kwenda kuziweka katika masanduku ya kupigia kura huku akionyesha karatasi hizo juu kabla ya kuzitumbukiza katika masanduku.
Alipomaliza kutumbukiza karatasi hizo, Dk. Magufuli alienda sehemu ya kupakwa wino kidoleni, ambapo baada ya kufanya hivyo alinyoosha juu kidole chake kuonyesha kwamba amekamilisha upigaji kura.
Baada ya kutoka ndani, Dk. Magufuli aliwapungia mkono wananchi waliokuwa katika foleni wakisubiri kupiga kura.
Akizungumza na waandishi wa habari, Dk. Magufuli alisema kwa ujumla anamshukuru Mungu ku?ka siku ya jana, ambapo Tanzania ime?ka wakati demokrasia inatakiwa ichukue mkondo wake.
“Nimetimiza wajibu wangu kama raia wa Tanzania kwa kupiga kura. Wito wangu kwa Watanzania ambao hawajaenda kupiga kura, wajihimu wakapige kura kuchagua viongozi wanaowataka kwa sababu hilo ni jukumu letu kuhakikisha demokrasia inakamilika. Tumtangulize Mungu,” alisema.
Wakati Dk. Magufuli akipiga kura katika kituo namba moja cha Shule hiyo, mkewe Janeth Magufuli alienda kupiga kura katika kituo namba tatu.
Muangalizi Mkuu: Uchaguzi ni huru na sa? Kata ya Kisutu jana ilitembelewa na Muangalizi Mkuu kutoka Umoja wa Ulaya, Judith Sargentini, ambaye alieleza kufurahishwa na mwamko mkubwa wa Watanzania ambao waliojitokeza kupiga kura katika kata hiyo.
Judith alisema kazi kubwa iliyowaleta ni kuona sheria za uchaguzi na taratibu zake zinafuatwa.
“Kila nchi ina taratibu zake katika kufanya uchaguzi, hivyo tupo hapa kwa ajili ya kuangalia iwapo taratibu hizo zinafuatwa,” alisema.
Alisema kati ya vituo walivyokagua wameona kuna hali kubwa ya utulivu na wananchi wanapiga kura kwa kufuata maelekezo ya wasimamizi wa vituo.
Katika kituo hicho, hali ilionekana kuwa shwari huku wasimamizi wa vituo wakionekana kutekeleza kazi yao ipasavyo.
Lowassa:Utaratibu Unaridhisha
Mgombea urais wa CHADEMA anayeungwa mkono na UKAWA, Edward Lowassa, alipiga kura Monduli mkoani Arusha.
Alisema ameridhishwa na utaratibu uliokuwepo na kwamba ulikuwa mzuri.
Hata hivyo, alisema hana maoni yoyote kuhusu, wananchi kukaa umbali wa mita 200 kulinda kura. Aliwataka wananchi kufuata taratibu na sheria zilizopo.
Shein avitaka vyama kukubali Matokeo
Rais wa Zanzibar Dk. Ali Mohammed Shein, amepiga kura katika Kituo cha Shule ya Msingi Bungi, kilichoko katika Jimbo la Tunguu, wilaya ya Kati, mkoa wa Kusini Unguja na kuvitaka vyama kukubali matokeo ya uchaguzi ili kuiepusha nchi na vurugu.
Dk. Shein ambaye pia ni mgombea urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), ali?ka katika kituo cha kupiga kura kama wananchi wengine huku kukiwa na hali ya utulivu na amani katika kituo hicho, alisema Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC), ipo kisheria na ndiyo yenye jukumu la kutangaza matokeo.
“Naviasa vyama vyote vikubali matokeo bila kujali kipi kimeshinda au kushindwa kwa lengo la kuzuia ghasia katika nchi,” aliasa Dk. Shein.
Dk. Shein ambaye ali?ka katika kituo cha kupigia kura saa 12:53 asubuhi, pia alisema maandalizi ni mazuri na ana amini watu wengi watapata nafasi ya kupiga kura kama yeye.
“Nimebahatika kuwa wa kwanza kupiga kura. Wananchi nao wajitokeze, maandalizi ni mazuri kila mtu atapata nafasi na wataridhika,” alisema Dk. Shein ambaye alikuwa na sura ya bashasha wakati alipokuwa akijibu maswali ya waandishi wa habari.
Mgombea huyo alisema akifanikiwa kurejea madarakani wananchi wategemee mafanikio makubwa na Zanzibar yenye matumaini zaidi.
Dk. Shein alisema kura ni siri, lakini haoni sababu ya ku?cha kwamba amejipigia mwenyewe na wagombea wengine wa chama chake, huku akionyesha wino uliokuwa kwenye vidole vyake baada ya kukamilisha mchakato huo.
JK aweka historia, apanga foleni
Ilipotimu saa 5.25 asubuhi, msafara wa magari ya Rais Jakaya Kikwete uli?ka kijijini Msoga, kwa ajili ya kumchagua rais ambaye atamrithi baada ya kukabidhi madaraka yake.
Baada ya ku?ka katika kituo cha kupigia kura, Rais Kikwete akiwa ameongozana na mkewe Mama Salma, alisalimia na watu waliokuwepo katika kituo hicho.
Alipo?ka alipanga foleni na kuamua kuvua koti lake na kuwapa wasaidizi wake. Imekuwa tofauti na mazoea kwa kuwa Rais Kikwete aliamua kupanga foleni na kuwa katika msururu wa watu ambapo alikaa kwa takriban dakika 10.
Hata hivyo, baada ya kukaa muda huo, katika foleni kama walivyokaa wananchi wengine, alipita mbele na kufuata utaratibu wa kuhakikiwa uwepo wa jina lake.
Baadae alichukua fomu ya kupiga kura yenye majina ya wagombea wa ngazi ya urais, ubunge na udiwani na baada ya hapo alienda katika chumba maalumu cha kuchagua viongozi hao.
Baada ya kupiga kura, aliingiza karatasi katika masanduku na baada ya hapo alihakikiwa kwa alama ya wino katika kidole kuonyesha kwamba ameshapiga kura.
Akizungumza na waandishi wa habari baada ya kupiga kura, Rais Kikwete alisema ametumia haki yake ya kupiga kura kama raia mwingine na kwamba hajapata taarifa ya manung’uniko.
“Zoezi la upigaji kura limekwenda salama na kwa utulivu. Naomba kusiwe na bughuza, Watanzania wachague viongozi wanaowataka kwa uhuru wao. Vituo Vyote kuna utulivu kama Msoga,” alisema Rais Kikwete.
Alitoa wito kwa wananchi kujitokeza kwa wingi kutumia fursa yao ya kupiga kura ambayo inatokea kwa miaka mitano.
Kuhusu ushindani wa vyama vya siasa wakati wa kampeni, Rais Kikwete alisema miaka yote ushindani ni mkali. Alisema mwaka 2005 na 2010, ushindani ni mkali na kuhoji kilichozidi mwaka huu ni nini.
“Leo (jana), tunamchagua Rais. Nimemaliza kazi, narudi kijijini kwangu. Mimi ni mfugaji pia nalima mananasi Kiwangwa. Nitaanzisha taasisi yangu inayojihusisha na mambo ya maendeleo ambayo nitasaidia nchi yangu. Nitakuwa rais mstaafu Novemba 5, mwaka huu,” alisema
Mkapa: Wagombea kubalini matokeoRais mstaafu wa awamu ya tatu, Benjamin Mkapa, alitumia haki yake ya Kikatiba, ambapo alikwenda kupiga kura katika Kata ya Kivukoni, akiwa ameongozana na mkewe Mama Anna.
Rais Mkapa ali?ka kituo cha Mkurabita, saa nne asubuhi, akiwa na mkewe, ambapo alisema amefurahi kutimiza haki yake ya kikatiba ya kupiga kura na kuwachagua viongozi anaowataka.
Alisema kila Mtanzania ana haki ya kupiga kura na kumchagua kiongozi anayemtaka, hivyo anafurahi kutimiza haki hiyo.
Pia, alisema amefurahi kuona upigaji kura unakwenda kwa utulivu mkubwa katika kituo chake na ana imani amani itaendelea hadi matokeo yatakapotangazwa.
Aidha, aliwataka wagombea wote kukubaliana na matokeo yatakayotangazwa hapo baadaee ili kuendelea kudumisha amani iliyopo.
“Ni wajibu wa kila kiongozi kukubali matokeo yatakayotangazwa ili kudumisha amani iliyopo kwa kuwa kila kiongozi ametangaza sera zake na kitakachoamriwa na wananchi kiheshimiwe na kila mgombea,” alisema Rais Mkapa.
Dk. Gharib afunguka
Makamu wa Rais, Dk. Mohammed Gharib Bilal ambaye alipiga kura katika kituo namba saba kwenye Shule ya Kiembe Samaki, Wilaya ya Magharibi B, Mkoa wa Mjini Magharibi, alisema uchaguzi wa mwaka huu una tofauti kubwa na uliofanyika 2010.
Alisema watu wamechangamka na kuhamasika ikiwemo baadhi ya vyama kuungana na kupunguza utitiri wa wagombea.
Dk. Bilal alisema pia mchakato wa upigaji kura umekwenda vizuri na kuwapongeza wasimamizi wote kwa kufanikisha hilo na kuahidi uchaguzi huo utakuwa huru, salama na haki kwa Zanzibar na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar, Balozi Seif Ali Idd, Rais wa Awamu ya Pili wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Ali Hassan Mwinyi ‘Mzee Ruksa’ na Dk. Salmin Amour ‘Komandoo’ ni miongoni mwa marais wastaafu waliopiga kura jana.
Samia:Naamini Tutashinda
Mgombea Mwenza wa urais kupitia CCM, Samia Suluhu Hassan ambaye alipiga kura katika kituo cha Kiembe Samaki jana saa 3.00 asubuhi alisema ana uhakika CCM itaibuka na ushindi katika uchaguzi huo.
Alisema ameridhishwa na hali ya utulivu katika vituo vya kupigia kura na kwamba mchakato utamalizika kwa amani na utulivu.
Samia alisema amefurahishwa na mwitikio wa watu wengi katika vityuo vya kupigia kura husan wanawake, ambao wengi walimuahidi kumuunga mkono kwa kuichagua CCM.
Pinda Mambo Safi
Waziri Mkuu Mizengo Pinda amesema anaamini kwamba uchaguzi wa Rais, wabunge na madiwani uliofanyika jana utakuwa wa amani na utulivu.
Akizungumza mara baada ya kupiga kura katika Kijiji cha Kibaoni, Wilaya ya Mlele, Mkoa wa Katavi, Pinda alisema hali ni nzuri.
“Watu wamejitokeza kwa wingi. Ninawasihi Watanzania waendelee kumuomba Mungu ili uchaguzi umalizike kwa amani,“ alisema.
Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari iliyotolewa jana na O?si ya Waziri Mkuu, ilisema Pinda aliwaasa wananchi kuendelea kumuomba mungu ili amani iliyoko nchini idumu.
Pinda alisema amefurahi baada ya ku?ka katika kituo chake cha kupigia kura na na kuona utaratibu mzuri uliopangwa wa kutenganisha wapigakura kutokan na jinsia.
“Nimekuta kina mama wana mistari yao, akinababa wana mistari na hapa kituoni kuna sehemu nne za kupigia kura,” alisema.
Alisema kwa wastani mtu mmoja anatumia dakika mbili tangu kuhakikiwa hadi kupiga kura na ni dalili njema inayoashiria watu kumaliza kupiga kura kwa wakati.
Aliwata kawapiga kura kote nchini wakimaliza kupiga kura waende majumbani kwao ikiwa ni kuitikia maelekezo ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi yanayowataka wananchi wasifanye mikusanyiko mita 200 kutoka kwenye kituo cha kupigia kura.
Naye msimamizi wa kituo hicho ambaye pia ni Mtendaji wa Kata ya Kibaoni, Thomas Senga, alisema watu wamejitokeza mapema kipiga kura tangu saa moja asubuhi.
Katika hatua nyingine, Pinda amevunja ukimya kuhusu taarifa zilizokuwa zinatolewa na baadhi ya watu kuwa ana mpango wa kuhama chama kwamba si sahihi.
Pinda alisema hajahama CCM kama ambavyo imekuwa ikidaiwa na baadhi watu na mitandao ya kijamii kwamba amejiunga CHADEMA.
Pinda alitoa kauli hiyo juzi alipozungumza na wananchi wa majimbo ya Mpanda Mjini na Kavuu kwenye mikutano minne ya hadhara iliyofanyika katika Kata za Kakese, Kibaoni, Usevya na Majimoto wakati akifunga kampeni za uchaguzi mkoani Katavi.
“Kuna picha zimesambaa mitandaoni zinadai nimehamia CHADEMA. Hivi kweli, sasa hivi nahamia huko ili iwe nini?” Alihoji na kushangiliwa na wakazi wa majimbo hayo.
Alisema picha wanazozisambaza ni za mwaka 2012 ambazo zilipigwa wakati akionyesha kwa wananchi moja ya kadi alizopokea kutoka kwa wanachama wa CHADEMA.
Katika moja ya picha hizo, Waziri Mkuu Pinda anaonekana akiwa na mlinzi wake huku akionyesha kadi ya CHADEMA.
Hakuna kiongozi yeyote wa CHADEMA anaye onekana akimkabidhi kadi kama mwanachama mpya.
Mgombea TLP akwama Kupiga Kura
Mgombea urais kupitia TLP, Macmillan Lyimo, ameshindwa kupiga kura baada ya kwenda katika kituo cha kupigia kura bila ya kuwa na kitambulisho cha kupigia kura.
Lymo alijiandikishia jijini Dar es Salaam na kufungia kampeni zake katika Jimbo la Vunjo mkoani Kilimanjaro juzi, alikwenda katika Kituo cha Ghalani kilichopo Njia Panda ya Himo.
Akizungumza na waandishi wa habari jana, alisema alishindwa kupiga kura kutokana na kutojiandikisha hapo, hivyo alitakiwa na msimamizi wa uchaguzi katika kituo hicho kujaza fomu maalum namba 18, itayomwezesha kupiga kura moja ya urais.
Na kuongeza kuwa: “Unajua jana nilichelewa kumaliza mikutano yangu ya kampeni kwani nilimaliza saa 12 jioni, hivyo nikaona kutoka na gari hapa mpaka Dar es Salaam kwa ajili ya Kwenda kupiga kura itakuwa tabu ndio maana nikaona ni bora nipigie huku huku Vunjo.”
Kwa upande wake, Msimamizi Mkuu wa Uchaguzi katika kituo hicho la Ghalani-Kilototoni namba mbili, Aliko Mkumbwa, alisema Lymo alifika kituoni hapo na kujieleza vizuri, ambapo alidai kuwa alijiandikishia Dar es salaam.
Mkumbwa aliendelea kudai kuwa mgombea huyo alidai kitambulisho chake cha kupigia kura amekisahau na kuomba kupiga kura, halafu arudi nyumbani kukichukua na kumletea kituoni ambapo ni kinyume na taratibu.
“Kutokana na kutokuwa na kitambulisho cha kupigia kura sikuweza kumruhusu apige kura na nilimtaka arudi kwanza nyumbani akachukue kitambulisho ndio aje kwa ajili ya kujaza fomu namba 18, ambapo nitamruhusu kupiga kura moja ambayo ni ya urais tu,” alisema Mkumbwa.

No comments:
Post a Comment