NA MWANDISHI WETU
CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kimeiomba Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), kutolea ufafanuzi propaganda hatarishi zinazosambazwa kwenye mitandao ya kijamii, kuhusu wizi wa kura ili kuepusha wananchi kutopotoshwa.
Aidha, kimesikitishwa na kauli ya Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe na Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi, James Mbatia, kwamba watatangaza matokeo yao na kuwaamuru vijana wao kuingia barabarani, kusherehekea.
Mbali na hilo, CCM, imesema uchaguzi umefanyika kwa amani ingawa kumejitokeza mapungufu kwenye maeneo kadhaa.
Akizungumza na waandishi wa habari jana, O?si Ndogo za CCM Makao Makuu, Lumumba, Dar es Salaam, Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa na Mjumbe wa Kamati ya Kampeni, Januari Makamba, alisema kuanzia juzi jioni hadi sasa, baadhi ya watu wanaeneza taarifa zikiambatanana picha, zinazotuhumu matukio ya wizi wa kura.
Januari alisema propaganda za aina hiyo ni hatari na kwamba zinafanyika zaidi kwenye mitandao ya kijamii.
Chama kinaiomba NEC kutopuuza matukio hayo na inapaswa kuyatolea ufafanuzi na maelezo ili kuepusha wananchi kutopotoshwa. “Propaganda hizo zinaweza kuhatarishaamani na usalama wa nchi,” alisema.
Januari alisema Chama kimesikitishwa na kauli ya Mbowe na Mbatia kuwa watatangaza matokeo yao na kuwataka vijana waingie barabarani kusherehekea.
“Mbowe alidai kuwa matokeo yao yasipofanana na yale yaliyotokana na kura za wananchi, hawatayakubali. Kauli hizi ni hatari sana kwa amani na usalama wa nchi na ujenzi wa demokrasia, zinapaswa kukemewa,” alisema Januari.
Alisema Chama kinashangazwa kuona hadi sasa Mbowe hajaitwa na kuhojiwa na mamlaka husika kwa kutoa tishio kwa amani ya nchi. Januari alisema viongozi wa upinzani wanasahau kuwa mahakama za kimataifa zina uwezo wa kuhukumu viongozi walio madarakani na hata walioko upinzani, ambao wanahamasisha fujo na vurugu.
Alisema CCM inalaani vikali kauli ya chama kimoja cha siasa kuamua kutangaza kuwa hakitakubali matokeo ya uchaguzi hata kabla ya matokeo hayajatangazwa.
“Chama kina sisitiza kuwa uamuzi wa Watanzania uheshimiwe na yoyote anayetaka kuvuruga amani ya nchi kwa kisingizo cha kutafuta madaraka, asivumiliwe,” alisema.
Alisema mgombea urais wa CCM, Dk. John Magufuli, leo atakuja Dar es Salaam, baada ya kupiga kura Chato.
Januari alisema Dk. Magufuli atatumia muda wake, kusubiri matokeo, kukutanana jopo lake na kuwashukuru wana-CCM, walioshirikiana naye katika kampeni.
Akizungumzia tathimini ya kupiga kura, Januari alisema yapo mapungufu yaliyojitokeza kwenye maeneo kadhaa na kuwa baadhi ya maeneo, upigaji wa kura ulichelewa, watu walipigana na maeneo mengine wasimamizi hawakujitokeza.
Januari alisema mapungufu hayo ni ya kiutawala na hayawezi kukisaidia chama chochote.
Alisema CCM inaitaka NEC kuhakikisha kila Mtanzania mwenye sifa ya kupiga kura anapata haki ya kufanya hivyo. Januari alisema Chama kinaviomba vyama vingine vitumie utaratibu rasmi wa kuwasilisha malalamiko ya uchaguzi.

No comments:
Post a Comment