Tuesday 17 November 2015

NDUGAI SPIKA MPYA WA BUNGE LA 11


HATIMAYE Naibu Spika katika Bunge la 10 la Jamhuri ya Muungano, Job Ndugai, amechaguliwa kuwa Spika mpya wa Bunge la 11.

Ndugai, ambaye ni mbunge wa Jimbo la Kongwa, alichaguliwa kushika wadhifa huo baada ya kupata kura 254, sawa na asilimia 70 ya kura 365 zilizopigwa.

Akitangaza matokeo hayo baada ya kumalizika kwa upigaji kura jana, Katibu wa Bunge, Dk. Thomas Kashililah alisema, mgombea wa CHADEMA, Goodluck Ole Medeye alipata kura 109.

Jumla ya wagombea wanane walishiriki katika uchaguzi huo, lakini mmoja alishindwa kufika Bungeni kuomba kura.

Katika uchaguzi huo, wagombea Hashim Rungwe wa CHAUMA, Peter Sarungi wa AFP, Dk. Godfrey Malisa wa CCK, Richard Lyimo wa TLP na Robert Kisinini wa DP hawakupata kura. Kura zilizoharibika zilikuwa mbili.

No comments:

Post a Comment