Friday, 22 January 2016

MAKAMU WA RAIS SAMIA ASHIRIKI DUA YA KUMUOMBEA MAREHEMU ASHA BAKARI MAKAME

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kulia, Mama Salma Kikwete katikati, Mama Mwanamwema  Shein kushoto na Wananchi wa Zanzibar, wakiwa katika Dua ya Pamoja ya kumuombea aliyekua Makamu Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake wa CCM Taifa (UWT) Marehemu Asha Bakari Makame iliyofanyika leo Januari 22,2016 nyumbani kwao Jang’ombe kabla ya mazishi yake yaliyofanyika katika kijiji cha Kianga Wilaya ya Magharibi Unguja.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kulia, Mama Salma Kikwete katikati, Mama Mwanamwema  Shein kushoto na Wananchi wa Zanzibar, wakiwa katika Dua ya Pamoja mbele ya Jeneza lenye Mwili wa aliyekua Makamu Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake wa CCM Taifa (UWT) Marehemu Asha Bakari Makame iliyofanyika leo Januari 22,2016 nyumbani kwao Jang’ombe kabla ya mazishi yake yaliyofanyika katika kijiji cha Kianga Wilaya ya Magharibi Unguja.

Baadhi ya Viongozi wa Serikali na Vyama vya Siasa wakishiriki kubeba Jeneza lenye Mwili wa aliyekua Makamu Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake wa CCM Taifa (UWT) Marehemu Asha Bakari Makame kabla ya mazishi yake yaliyofanyika  leo Januari 22,2016 katika kijiji cha Kianga Wilaya ya Magharibi Unguja

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kushoto akizungumza na kuwafariji wanafamilia wa aliyekua Makamu Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake wa CCM Taifa (UWT) Marehemu Asha Bakari Makame baada ya Dua maalum iliyofanyika leo Januari 22,2016 nyumbani kwao Jang’ombe, Mhe. Asha amezikwa leo kijijini kwake Kianga Wilaya ya Magharibi Unguja.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kulia akimfariji Mama Mzazi wa aliyekua Makamu Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake wa CCM Taifa (UWT) Marehemu Asha Bakari Makame, Bibi Mwanajuma Faki (90) wakati wa Dua maalum iliyofanyika leo Januari 22,2016 nyumbani kwao Jang’ombe Zanzibar, Mhe. Asha amezikwa leo kijijini kwake Kianga Wilaya ya Magharibi Unguja.

No comments:

Post a Comment