Friday, 29 January 2016

SERIKALI KUTAIFISHA MAHEKALU NA MALI ZA MAFISADI




SERIKALI imetangaza kiama kwa kutaifi sha mali za watu watakaobainika na makosa ya uhujumu uchumi, wakiwemo mafi sadi, majangili, wafanyabiashara wa dawa za kulevya na watuhumiwa wa makosa ya rushwa.

Hatua hiyo ni muendelezo wa mikakati yake ya kuwashughulikia wahalifu katika namna mbalimbali ambapo, kwa sasa imetangaza kutaifi sha mali zao. 


Imesema kuwa licha ya adhabu nyingine zinazotolewa na mahakama, pia watakaothibitika kuhujumu uchumi mali zao zitataifi shwa na kuwa za umma.

Tayari serikali imeshakusanya sh. bilioni 11 za wahalifu mbalimbali waliofanya makosa yanayohusiana na ufi sadi, dawa za kulevya, ujangili na rushwa. 


Mbali na fedha hizo, ambazo zimerejeshwa serikalini, pia serikali imetaifi sha baadhi ya majumba makubwa, magari na viwanja vilivyokuwa vikimilikiwa na watuhumiwa hao, ambao wengine.

wameshashitakiwa na kupewa hukumu. Akizungumza na waandishi wa habari jana, Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Mashitaka Nchini (DPP), Biswalo Mganga, alisema lengo la serikali ni kupigana na wahalifu ili mali zote zinazotokana na uhalifu zirudishwe mikononi mwake.

Mganga alisema suala la kutaifi sha mali za waharifu lipo tangu 1990 na limetungiwa sheria, hivyo kitakachofanyika ni utekelezaji tu wa sheria husika. 


Alisema licha ya fedha walizokusanya, tayari kuna nyumba na magari matano, ambayo yamerudi mikononi mwa serikali.

Mkurugenzi huyo aliyataja makosa, ambayo kesi zake zimeshamalizika mahakamani, zinazohusiana na dawa za kulevya na ujangili na tayari wahusika wameshatoa faini na wengine kutaifi shwa mali zao .

Miongoni mwa kesi hizo ni iliyohukumiwa na Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Moshi, iliyowahusisha washitakiwa wawili, ambao ni Musa Ramadhani, aliyekamatwa na dawa za kulevya aina cocaine kilo tatu, zenye thamani ya sh. milioni 100 na kufungwa kifungo cha maisha jela.

Mshitakiwa mwingine ni Hamisi Ramadhani, aliyekamatwa na dawa za kulevya aina heroine kilo tatu, zenye thamani ya sh. milioni 143, ambaye pia amehukumiwa kifungo cha maisha jela.

Alisema washitakiwa hao watafilisiwa na mali zao kurudi mikononi mwa serikali kwa mujibu wa sheria. 


Katika kesi nyingine ya ujangili, raia wa Qatar alikamatwa akiwa na pembe mbili za Twiga, ambapo alihukumiwa kulipa faini ya sh. milioni 64.

Pia, raia wa Marekani, John Jon alikamatwa akiwa na pembe mbili za Twiga nakuhukumiwa faini ya sh. milioni 64. 


Katika kesi nyingine, mshitakiwa Hussein Masuid, ambaye ni Mtanzania, alikamatwa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar es Salaam, akiwa na kobe 133, alihukumiwa faini ya sh. milioni 54.

Mwingine ni raia wa China, amehukumiwa kulipa faini ya sh. milioni 68 baada ya kukutwa na meno ya kifaru 11.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI), Diwani Athumani, alisema upelelezi unaofanywa nchini unafanyika katika mataifa yote duniani. 

Alisema mhalifu yeyote akipatikana na makosa ya ufi sadi, rushwa na ujangili ni lazima mahakama imuhukumu na kutaifi shwa mali zake ili zirudi mkononi mwa serikali.

DCI Athumani alisema kumkamata mhalifu na kumhukumu bila ya kutaifi sha mali zake, hakuna tija kwa taifa kwa kuwa akimaliza kifungo atazikuta na kuendelea kuzitumia kama kawaida.

Aliongeza kuwa tayari polisi imekamilisha upelelezi wa kesi 23, ambazo ziliwasilishwa kwa DPP na kati ya hizo, tatu zimetolewa uamuzi na nyingine 20, ziko katika hatua ya maombi ya kupata amri ya mahakama ili ziweze kuzuiwa au kutaifi shwa .

Alisema mali zinazohusiana na uchunguzi huo ni pamoja na nyumba, viwanja, magari, boti na fedha taslimu.

Pia, alisema sheria hiyo itashughilikia wahalifu wote bila kujali nyadhifa zao, ambapo hata kama mtuhumiwa ni mwanasiasa au mtu yeyote maarufu, atahukumiwa na kufi lisiwa mali alizonazo.

Mkurugenzi wa Upelelezi kutoka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), Alex Mfungo, alisema uhalifu hauwezi kumalizika iwapo muhusika amehukumiwa kutumikia kifungo huku mali zake zikiwa uraiani.

Mfungo alisema hivi sasa wameamua kufanyakazi kwa pamoja na DPP na DCI ili wahalifu wote wanaokamatwa waweze kurudisha mali zao mikononi mwa serikali.

Alisema ndani ya TAKUKURU, wameanzisha kitengo maalumu cha urejeshaji wa mali zote zilizopatikana kwa njia isiyo halali, ikiwa ni pamoja na njia ya rushwa.

Hata hivyo, alisema watafanyakazi kwa mujibu wa sheria bila ya kumuogopa au kumuonea mtu yeyote.

No comments:

Post a Comment