Sunday, 31 January 2016
WAWINDAJI HARAMU WATUNGUA HELIKOPTA NA KUUA RUBANI WAKE,WADAIWA KUUA TEMBO WATATU PORI LA AKIBA MKOANI MASWA.
Watu wanaodaiwa kuwa ni majangili na wawindaji haramu wameitungua kwa risasi helkopta hiyo ya doria na kumuua rubani wake raia wa Uingereza katika pori la akiba la Maswa mkoani Simiyu.
Katika tukio hilo ambalo pia lilimjeruhi askari wa wanyamapori, helkopta hiyo mali ya kampuni ya uhifadhi iitwayo Friedkin Conservation Fund ilikuwa katika doria kwenye pori la uwindaji wa kitalii la Mwiba.
Tukio hili la majangili kutungua helkopta kwa risasi ni la kwanza kutokea katika historia ya uhifadhi nchini Tanzania na imeelezwa kuwa doria hiyo ilikuwa inafanyika kufuatia milio ya risasi iliyotokea katika eneo hilo la pori la akiba la Maswa ambapo majangili hao walikuwa wameuwa tembo watatu na kuchukua meno yao.
Waziri wa Maliasili na utalii Profesa Jumanne Maghembe amefika katika eneo la tukio na amesema Serikali inaanzisha mkakati mpya wa kupambana na ujangili na maharamia hao waliotungua helkopta hiyo na kusababisha kifo cha rubani lazima wakamatwe- picha na Vedasto Msungu Technologies.
Waziri wa Maliasili na utalii Profesa Jumanne Maghembe akifafanua jambo kwenye tukio hilo
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment