Monday, 21 March 2016

BREAKING NEWSSSSSSS..DK SHEIN ASHINDA URAIS ZANZIBAR

Aliyekuwa Mgombea Urais wa Zanzibar kwa tiketi ya CCM, Dkt. Ali Mohammed Shein akikabidhiwa cheti cha Ushindi kutoka kwa Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC), Jecha Salum Jecha, mara baada ya kutangazwa mshindi wa uchaguzi wa urais Zanzibar akiwa na kura 299,982.
Aliyekuwa Mgombea Urais wa Zanzibar kwa tiketi ya Chama cha ADC, Hamad Rashid Mohamed ndiye alieshika nafasi ya pili akiwa na kura 9,734.
 

Matokeo kamili kama yalivyotangazwa na Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC), yanaonyesha licha ya Chama cha Wananchi (CUF) kususia, mgombea wake Maalim Seif Sharif Hamad alipata kura 6,076 kwenye uchaguzi wa marudio uliofanyika Jumapili.

Kulikuwa na wagombea 14 kwenye karatasi za kura za kumchagua Rais. Majina yao ndiyo haya:
 

1 Khamis Iddi Lila ACT-W
2 Juma Ali Khatib ADA-TADEA
3 Hamad Rashid Mohamed ADC
4 Said Soud Said AFP
5 Ali Khatib Ali CCK
6 Ali Mohamed Shein CCM
7 Mohammed Massoud Rashid CHAUMMA
8 Seif Sharif Hamad CUF
9 Taibu Mussa Juma DM
10 Abdalla Kombo Khamis DP
11 Kassim Bakar Aly JAHAZI
12 Seif Ali Iddi NRA
13 Issa Mohammed Zonga SAU
14 Hafidh Hassan Suleiman TLP

No comments:

Post a Comment