Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amemtumia salamu za
rambirambi Mkuu wa Mkoa wa Njombe Dkt. Rehema Nchimbi, kufuatia kifo cha ghafla
cha Mkuu wa Wilaya ya Njombe Bi. Sara Dumba, Kilichotokea jana jioni tarehe 21
Machi, 2016.
Bi.
Sara Dumba aliugua ghafla kuanzia jana mchana na baadaye kukimbizwa katika
hospitali ya Mkoa wa Njombe (Kibena), ambako wakati akipatiwa matibabu
alifariki dunia majira ya saa moja za jioni.
Katika
salamu hizo Rais Magufuli ameelezea kushitushwa na kifo cha ghafla cha Bi. Sara
Dumba, ambaye amesema alimfahamu kwa uchapakazi wake, uaminifu na uadilifu
katika utumishi wa umma na katika uongozi.
“Nimeshitushwa
sana na kifo cha Mkuu wa Wilaya ya Njombe Bi. Sara Dumba, kwa mara nyingine
Taifa limempoteza mtu muhimu ambaye mchango wake ulikuwa bado unahitajika”
amesema Rais Magufuli.
Dkt.
Magufuli amebainisha kuwa Marehemu Sara dumba atakumbukwa kwa kazi kubwa
aliyoifanya ya kuhimiza maendeleo ya wananchi, hususani katika kilimo na
ufugaji, kuhimiza nidhamu ya utumishi serikalini na kuwatetea wananchi wa hali
ya chini wakati wote wa majukumu yake ya ukuu wa wilaya.
Rais
Magufuli amesema anaungana na familia ya marehemu, ndugu, jamaa, marafiki na wote
walioguswa na msiba huu mkubwa, katika kipindi hiki kigumu na pia amewataka
wote kuwa na subira na uvumilivu.
Amemuombea
kwa Mwenyezi Mungu aipumzishe roho yake mahali pema peponi, Amina.
Gerson
Msigwa
Kaimu
Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Dar
es salaam
22
Machi, 2016
No comments:
Post a Comment