Amtaka Mkurugenzi wa Bandari aandae dispatch zote tangu 2014
Naibu Waziri Ujenzi aagiza kampuni za forodha zifunguliwe
WAZIRI
MKUU Kassim Majaliwa amemuagiza Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali aende
Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) ili akague taarifa za mapato ambazo zilikuwa
zikilipwa na mawakala wa forodha na bandari kupitia benki ya CRDB lakini
hazionekani kwenye mifumo ya benki.
Ametoa
agizo hilo leo jioni (Jumatatu, Machi 21, 2016) wakati akizungumza na mamia ya
mawakala wa forodha na bandari waliohudhuria mkutano aliouitisha ili kusikiliza
kero zinazowapata katika utendaji kazi wao.
Akizungumza
na mawakala hao kwenye ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam, Waziri Mkuu
alisema kuna dalili za kutupiana lawama baina TPA na CRDB kuhusu malipo
yaliyikuwa yakifanyika benki halafu fedha hazionekana na wakala anaidaiwa kuwa
hajalipia mzigo wakati alishaulipia.
“Kimsingi
bado liko tatizo baina ya Mamlaka ya Bandari pamoja na Benki ya CRDB. Naona
kila mmoja hapa anamkana mwenzake. Nitamtuma CAG ili akafanye ukaguzi wa kina
ili tujue ni nani kati yao amehusika na upotevu wa fedha,” alisema huku
akishangiliwa na mawakala hao.
Alimwagiza
pia Kaimu Mkurugenzi wa Bandari, Eng. Aloyce Matei aandae dispatch zote
walizotumia kupokelea malipo za kuanzia mwaka 2015 na ikibidi aandae za kuanzia
mwaka 2014 ili CAG anapozopitia aweze kupata picha halisi.
Vilevile,
Waziri Mkuu alimwagiza Eng. Matei kuhakikisha wananunua mashine ya photocopy
ili iwekwe kwenye chumba cha kupokelea stakabadhi za malipo ya benki (bank pay
in slip) ili mteja anapoleta nakala ya benki aweze kutolewa photocopy na
kubakia na nakala ya malipo aliyofanya,
Waziri
Mkuu alisema Serikali inatambua bandari ni eneo nyeti katika kuinua uchumi na
mapato ya nchi lakini pia ni eneo muhimu katika kutengeneza ajira. “Ninapenda
niwahakikishie kuwa bado tutaendelea kukagua bandari hadi pawe safi. Hii
bandari ni yenu na mtafanya kazi kama kawaida,” alisema.
Mapema,
akizumgumza kwa niaba ya mawakala hao, Rais wa Chama cha Mawakala wa Forodha
nchini (TAFFA), Bw. Stephen Ngatunga alieleza matatizo mbalimbali ambayo wao
kama mawakala wa forodha wamekuwa wakikumbana nayo kuanzia ulipaji, utoaji wa
mizigo na kuitaka Serikali iongeze nguvu katika kuikabilia sekta hiyo.
Alizikosoa
baadhi ya sheria ambazo zinaruhusu wamiliki wa bandari kavu kumiliki pia
makampuni ya uwakala wa forodha, sheria kadhaa zinazochangia kukwamisha utoaji
wa mizigo bandarini, ukaguzi hafifu wa kwenye scanner na uwepo wa vituo vinane
vya mizani kuanzia Dar es Salaam hadi Tunduma ambavyo vimegeuka kuwa kero kwa
wasafirishaji wa mizigo kwenda nchi jirani.
Wakati
huohuo, Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Eng. Edwin Ngonyani
amesema Serikali imeamua kuyafungulia makampuni zaidi ya 150 ambayo yalikuwa
yamefungiwa kufanya kazi za uwakala wa forodha kutokana na madai ya kuhusishwa
na ukwepaji wa kodi.
“Hapa
tumegundua kuwa wote siyo wasafi iwe ni mawakala, benki ama bandari. Mkurugenzi
wa Bandari, kuanzia leo watu hawa waruhusiwe waanze kufanya biashara lakini
nyaraka za nyuma zisiguswe hadi CAG atakapokamilisha uchunguzi wake,” alisema kuibua
kelele za shangwe kwenye ukumbi huo.
IMETOLEWA
NA:
OFISI
YA WAZIRI MKUU
2
MTAA WA MAGOGONI,
- L. P. 3021,
11410
DAR ES SALAAM
JUMATATU,
MACHI 21, 2016.
No comments:
Post a Comment