Tuesday 31 May 2016

CCM KUBORESHA KANUNI ZA UTUMISHI


 


NAIBU Katibu Mkuu wa CCM (Bara) Rajabu Luhawvi, amesema Chama  kinatarajia kufanya maboresho makubwa ya kanuni ya watumishi wake.

Amesema CCM itaondoa vipengele ambavyo havizingatii mazingira yalioko sasa na kwamba, mabadiliko hayo yatajali haki kwa watumishi wake.

“Miongoni mwa vipengele hivyo ni gharama za usafirishaji wa mizigo kwa watumishi wanaostaafu na kwamba, tutapandisha kiwango kizuri kwa maslahi ya watumishi wetu,”alisema Luhwavi.

Luhawvi amesema kwa upande wa kipengele cha michango ya rambirambi kwa wazazi wa watumishi, itazingatiwa kwa jicho la umakini zaidi, ambapo awali ilikuwa inatambua familia ya mke, mume na watoto.

Alisema suala lingine ni marekebisho ya sheria ya watumishi wa Chama ya mwaka 2004 na 2006,  ambayo inamtaka mtumishi aliyesimamishwa kazi kulipwa nusu mshahara na kwamba,
kwa sasa itafanyiwa marekebisho.

“Katika eneo la mafunzo la watumishi pia litafanyiwa marekebisho kwa kutoa mafunzo kwa wafanyakazi bila kujali nafasi ya mfanyakazi, hivyo kuna haja ya kutoa mafunzo ya itikadi kwa lengo la kuimarisha CCM,”alisema

Alisema CCM inatarajia kufanya mabadiliko makubwa kwa watumishi wake na kuwaasa kujiendeleza katika taaluma za masomo ili kuongeza ufanisi katika kazi za Chama.

“Ili CCM yetu ifikie matarajio ya mabadiliko ya kisasa, lazima tuongeze ujuzi wa taaluma zetu kwenda kisasa zaidi na jambo hilo litasaidia sana kuboresha CCM,” alisema.

Alisema watumishi, ambao wanachelewa kuajiriwa, watapata fursa nzuri kuajiriwa na kwa watumishi katika sekta ya usafiri, madereva, wataboreshewa mazingira ya kazi, ikiwemo mishahara na uhakika wa ajira.

No comments:

Post a Comment