Tuesday 31 May 2016

SAMIA AMWAKILISHA RAIS MAGUFULI MKUTANO WA KIMATAIFA

MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, akisalimiana na Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje wa Belize, Wilfered Eliringron, alipowasili kwenye Hoteli ya Airways, mjini Papua New Guinea. Samia nchini Papur New Guinea, kumwakilisha Rais John Magufuli, katika mkutano wa siku mbili, unaoanza leo, utajadili masuala ya kukuza usawa na maendeleo endelevu na utahudhuriwa na wakuu wa nchi za Afrika, Caribbean na Pacific (ACP).
MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Samia Suluhu Hassan, akizungumza na Mwandaaji Mkuu wa Mkutano wa The HL MEETING UN WOMEN, unaotarajiwa kufanyika keshokutwa mjini Guinea.  Makamu wa Rais yupo Papur New Guinea, kumwakilisha Rais John Magufuli katika mkutano wa siku mbili, unaotarajiwa kuanza leo, ambao utajadili masuala ya kukuza usawa na maendeleo endelevu na utahudhuriwa na wakuu wa nchi za Afrika, Caribbean na Pacific (ACP).

No comments:

Post a Comment