Sunday, 5 June 2016
TANZANIA ITAJENGWA NA WASOMI
RAIS Dk. John Magufuli, amesema anawapenda wanafunzi wa vyuo vikuu kwa kuwa anaamini wao ndiyo wataleta mabadiliko ya kweli ya kimfumo hapa nchini.
Pia amewaahidi wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, kuwa serikali itatoa sh. bilioni 10 kwa ajili ya ujenzi wa mabweni chuoni hapo, kutokana na changamoto ya malazi inayowakabili.
Hata hivyo, alitoa sharti ya mabweni hayo kujengwa katika maeneo ya chuo, badala ya maeneo hayo kuwapa wawekezaji.
“Nawapenda sana wanafunzi wa vyuo vikuu na nipo tayari kuhakikisha tunatatua changamoto
zinaziwakabili…hata hivyo msikubali kutumika na wana siasa, hasa kwenye mambo ya msingi ya kitaifa,” alisema Rais Magufuli.
Aliongeza kuwa: “Naawataka msome kwa bidiii, acheni siasa,.. mmekuja kusoma, someni, siasa mtaikuta mkimaliza shule, ninawaahidi tutajitahidi kutatua matatizo yetu bila
kujali itikadi za vyama.”
Aliyasema hayo jana, wakati alipokuwa akiweka jiwe la msingi katika ujenzi wa maktaba ya kisasa ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, inayojengwa kwa msaada wa Serikali ya China.
Vile vile, amesisitiza kuwa ni lazima Watanzania wasimamie sheria na utaratibu ili mambo yaende vizuri, hayupo tayari kuvumilia ukiukwaji wa sheria, vinginevyo amekusudia kutumbua majipu kila kukicha.
“Tumewajengea mbiundombinu ya barabara, utakuta watu wanajisaidiahuko, wengine wanapitisha magari yao katika barabara za mwendokasi, wakati wana barabara zao…polisi wapo, mkuu wa mkoa yupo, wakuu wa wilaya wapo, kwanini watu hawa wasikamatwe na kupelekwa jela kujisaidia,” alisema Magufuli na kusababisha watu kuangua kicheko.
Aidha, alisema Watanzania wanapaswa kutambua kuwa hivi sasa taifa lipo katika kipindi cha mabadiliko na kutaka watambue mabadiliko yana gharama zake, ikiwemo faida na hasara.
Alisema kwa mujibu wa taarifa alizonazo, zaidi ya asilimia 70 ya wanafunzi wa chuo hicho wanaishi wanakofahamu wao ambapo wanafunzi zaidi ya 3000 wanaishi chuoni hapo na 4000 katika hostel za Mabibo.
“Mpaka sasa eti kuna watu hawataki kubadilika ni mambo mengi ya ajabu yanafanyika, utakuta mtu anao wafanyakazi 10 hewa, wakati kuna wahitimu wanasota mitaani bila ajira,” alisema.
Vile vile, alisema wengine wanakiuka sheria kwa kudahili watu wasio na sifa ama wanafunzi hewa, ambapo serikali inatumia fedha nyingi kuwasomesha huku waliofaulu kwa viwango vya juu wakikosa nafasi za masomo, hususani mikopo.
“Wengine wamemaliza kidato cha nne na kupata daraja la nne, halafu wamepewa mikopo na nafasi ya kusoma vyuo vikuu na hao ni watoto wa wakubwa, ilhali waliomaliza kidato cha sita na kufaulu vizuri, watoto wa masikini kukosa mikopo,” alisema.
Aidha, alimpongeza Waziri wa Elimu, Sayansi na Mafunzo ya Ufundi, Joyce Ndalichako, kwa hatua ya kuwafukuza chuo wanafunzi hao wasio na vigezo na kusema Serikali inachambua upya kuangalia wenye sifa, ili kuwapa nafasi vyuoni na mkopo wa masomo.
“Halafu eti baadhi ya wanasiasa wanajitokeza na kuanzia kuwatetea, Mara oo hawana mahali pa kulala ni ujinga, tunapaswa kutanguliza uzalendo mbele, ndipo sasa ifuate, badala ya kuunga mkono mambo yasiyo na tija,” alisema.
Alisema kupitia kampeni yake ya ‘hapa kazi tu’ anahitaji umoja na kila mtu katika eneo lake la kazi kutimiza wajibu wake ili kulifi kisha taifa pale alipokusudia.
Rais alisema changamoto kubwa nchini ni mshikamano, ambapo ni muhimu kuweka umoja katika mambo yenye tija kwa taifa ili kuleta maendeleo.
Naye Makamu Mkuu wa Chuo hicho, Profesa Rwekaza Mukandala, akizungumza katika hafl a hiyo alisema maktaba hiyo itagharimu sh. bilioni 80.
Alisema maktaba hiyo itakuwa kubabwa barani Afrika na itasaidia kukuza kiwango cha elimu chuoni hapo.
Watu na viongozi mbalimbali waliowahi kusoma katika chuo hicho, akiwemo Mkuu wa Chuo, Dk. Jakaya Kikwete walihudhuria tukio hilo.
Akizungumza, Kikwete alisema hali ya chuo hicho si nzuri, hususan miundombinu na alimwomba Rais Magufuli kuhakikisha
kinakarabatiwa na kuongeza majengo kulingana na uhiataji, kwa kuwa idadi ya wanafunzi wanaoingia sasa ni kubwa.
Magufuli aliahidi kutatua changamoto hizo na kumsifu Kikwete wakati wa utawala wake alihakikisha elimu ya juu inapewa kipaumbele.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment