Sunday, 3 July 2016

RAIS DKT. MAGUFULI ASHIRIRKI DHIFA YA KITAIFA NA MGENI WAKE RAIS KAGAME.

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli (kulia) akigonganisha bilauri na Mke wa Rais wa Rwanda, Mama Jeannette Kagame katika kusherehekea Dhifa ya Kitaifa aliyomuandalia mgeni wake Rais wa Rwanda Paul Kagame (katikati) Ikulu jijini Dar es Salaam. Rais Kagame alikuwa nchini kwa ziara ya Kikazi.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan (kulia) akigonganisha bilauri na Rais wa Rwanda Paul Kagame, katika kusherehekea Dhifa ya Kitaifa iliyoandaliwa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwa ajili ya mgeni wake Rais Kagame.
Dhifa hiyo ilifanyika Ikulu jijini Dar es Salaam jana usiku.
    Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli (kulia) akifurahia jambo na mgeni wake Rais wa Rwanda Paul Kagame.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli (katikati) akiwa amesima kutoa heshima wakati wa Dhifa ya Kitaifa aliyomuandalia mgeni wake Rais Kagame (kulia kwake). Kulia ni Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan. Wa pilikulia ni Mke wa Tanzania Mama Janet Magufuli na kushoto ni Mke wa Rais wa Rwanda, Jeannette Kagame.
 Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili Alhaj Ali Hassan Mwinyi (wa tatu kushoto) akiwa na Waziri Mkuu Mstaafu Dkt Salim Ahmed Salim (wa pili kushoto), Jaji Mkuu wa Tanzania Mohamed Chande Othman (wa tatu kulia) Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Kikanda na Kimataifa, Balozi Dkt. Augustine Mahiga na Waziri wa Mambo ya Nje wa Rwanda, Louise Mushikiwabo (kulia).
  Waziri Mkuu Mstaafu Jiji Mstaafu Joseph Sinde Warioba akimsikiliza Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri Dkt. Tulia Ackson wakiwa kwenye Dhifa ya Kitaifa iliyoandaliwa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwa mgeni wake Rais Kagame. Dhifa hiyo ilifanyika Ikulu jijini Dar es Salaam.
 Jaji Mkuu wa Tanzania, Mohamed Chande Othman (kulia) akizungumza na  Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dar es Salaam, Ramadhani Madabida wakiwa kwenye Dhifa ya Kitaifa iliyoandaliwa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwa ajili ya mgeni wake Rais wa Rwanda Paul Kagame aliyetembelea Tanzania kwa ziara ya Kikazi.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Waziri Mkuu mstaafu Salim Ahmed Salim Ikulu jijini Dar es Salaam mara baada ya kumalizika kwa dhifa ya kitaifa aliyomwandalia Rais wa Rwanda Paul Kagame.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Rais Mstaafu wa awamu ya pili Alhaji Ali Hassan Mwinyi Ikulu jijini Dar es Salaam mara baada ya kumalizika kwa dhifa ya kitaifa aliyomwandalia Rais wa Rwanda Paul Kagame.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akijadiliana jambo na Mawaziri wakuu wastaafu, Jaji Joseph Sinde Warioba na Salim Ahmed Salim Ikulu jijini Dar es Salaam mara baada ya kumalizika kwa dhifa ya kitaifa aliyomwandalia Rais wa Rwanda Paul Kagame, Kulia ni mke wa Rais Mama Janeth Magufuli.

No comments:

Post a Comment