Sunday, 28 August 2016

MAJALIWA KUHAMIA RASMI DODOMA SEPTEMBA MOSI


WAZIRI Mkuu, Kasim
Majaliwa, Septemba Mosi,
mwaka huu, atahamia rasmi
mjini hapa, ambapo atapokelewa
na uongozi wa mkoa katika
eneo la Mtimba, nje kidogo ya
Manispaa ya Dodoma.
Hayo yalielezwa mjini
hapa jana na Mkuu wa Wilaya
ya Dodoma Mjini, Christina
Mndeme, wakati wa mkutano
wake na viongozi wa dini,
uliofanyika katika ukumbi wa
Hoteli ya Dodoma.
Alisema baada ya Waziri
Mkuu kupokelewa katika
eneo la Mtimba, msafara wake
utaelekea Uwanja wa Jamhuri,
ambako atazungumza na
wananchi wa Dodoma.
Christina alitumia nafasi
hiyo kuwaomba viongozi hao
wa dini kuungana na uongozi
wa wilaya kwenye mapokezi ya
Waziri Mkuu.
Alisema Waziri Mkuu
anahamia rasmi mjini hapa kwa
ajili ya makazi na kuendesha
shughuli zake mbalimbali,
ikiwemo za Chama na Serikali.
‘Kuhamia kwa waziri mkuu
ndio kuhamia kwa serikali,
hivyo tushirikiane kwa pamoja
kufanya kazi na viongozi wetu,
lakini pia kupokea wageni,
ambao ni waumini wa dini ya
kikristo na kiislamu,”alisema.
Katika hatua nyingine, Ofi si
ya Waziri Mkuu Sera, Uratibu
na Bunge, imesema ukarabati
wa nyumba ya Waziri Mkuu
upo katika hatua ya mwisho
kukamilika.
Hatua hiyo ilibainika baada
ya Waziri wa Nchi Ofi si ya Waziri
Mkuu Sera, Uratibu na Bunge,
Jenista Mhagama, kutembelea
na kukagua maendeleo ya
ukamilishaji huo, ikiwa ni agizo
lililotolewa na Waziri Mkuu,
Kassim Majaliwa hivi karibuni
mjini hapa.
Akizungumza baada
ya kukagua ukarabati huo,
Mhandisi wa Ofi si ya Waziri
Mkuu, Joseph Mhamba, alisema
shughuli zote za ukarabati
zinazofanywa na Wakala wa
Majengo (TBA), zinaendelea
vizuri.
Mhandisi huyo alifafanua
kuwa, kwa upande wa huduma
ya maji ya uhakika, inaendelea
kushughulikiwa huku akisema
kwa upande wa mawasiliano,
kampuni ya simu inaendelea
kusimika nguzo na kujenga
maeneo ya ukaguzi wa wageni.
Alisema kwa upande wa
ofi si kwa ajili ya watumishi, kazi
inaendelea vizuri.
‘Baada ya ukaguzi huu,
watafanya tathmini ili wajue
ukarabati wote umegharimu
kiasi gani cha fedha,’alisema.
Kwa upande wake, Jenista
alisema dhamira ya serikali
kuhamia Dodoma, inaendelea
kujidhihirisha na juhudi
zinafanyika kuhakikisha Waziri
Mkuu anahamia Dodoma,
Septemba kama alivyoahidi.
Aliwataka Watanzania
waendelee kuwaombea ili azma
hiyo inayotokana na Ilani ya
Uchaguzi ya CCM na ndoto ya
Baba wa Taifa Hayati Mwalimu
Julius Nyerere kutaka Dodoma
kuwa makao makuu, itimie.
Alisema uamuzi wa Waziri
Mkuu kuhamia Dodoma upo
pale pale na mafundi wako kazini
kuhakikisha kazi inakamilika
kama ilivyopangwa.
Naye Naibu Waziri Ofi si ya
Waziri Mkuu, Kazi, Vijana na
Ajira, Antony Mavunde, alisema
uamuzi wa kuhamia makao
makuu umeifanya serikali ya
awamu ya tano kutimiza ndoto
ya muda mrefu.
Naibu Waziri, Ofi si ya Waziri
Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana,
Ajira na Watu Wenye Ulemavu,
Dk. Abdallah Possi, alisema Rais
wa awamu ya tano Dk. John
Magufuli, amesikia kilio cha
Watanzania, ambao kwa muda
mrefu walikuwa wakihoji kwa
nini kila kitu kifanyike Dar es
Salaam, wakati makao makuu ni
Dodoma, huku ofi si za serikali
zikiendelea kujengwa Dar es
Salaam.
Mhandisi wa Ofi si ya
Waziri Mkuu, Joseph Mhamba
alisema kazi zinakwenda
vizuri na zitakamilika kama
zilivyopangwa.
Mhandisi Kashimilu
Mayunga kutoka Mamlaka ya
Majisafi na Usafi wa Mazingira
Dodoma Mjini (DUWASA),
alisema kazi inayoendelea ni
kuchimba mitaro na kulaza
mabomba.
Alisema kazi hiyo
imekamilika kwa zaidi ya
asilimia 70 na wanachosubiri
kwa sasa ni pampu.
Meneja mtandao wa Shirika
la Simu Tanzania (TTCL), Flavian
Mziray, alisema kwa sasa
wanamalizia kusimika nguzo
za simu, ambapo mpaka sasa
nguzo 21 tayari zimeshasimikwa
na bado nguzo tano.

No comments:

Post a Comment