Sunday, 28 August 2016

POLISI 80 WAONGEZWA MSAKO WA KUWASAKA MAJAMBAZI


MAPAMBANO ya
kuwasaka watuhumiwa wa
ujambazi yanayoendelea
Vikindu, Mkuranga, mkaoni
Pwani, yanaonekana kuwa
bado ni tete, ambapo Jeshi
la Polisi Kanda Maalumu ya
Dar es Salaam, limeongeza
askari 80 kwa ajili ya
kuongeza nguvu.
M a p a m b a n o
hayo yaliyoanza juzi,
yamesababisha mauaji ya
askari polisi na majambazi
kadhaa huku wengine
wakitiwa mbaroni.
Akizungumza na
waandishi wa habari, Dar es
Salaam, jana, Kamishna wa
Polisi Kanda Maalumu ya
Dar es Salaam, Simon Sirro,
alisema askari hao watafanya
oparesheni katika maeneo
mengi katika mkoa huo.
“Kuna majambazi
kadhaa wamekamatwa
na wengine wamekufa,
ambapo leo (jana) askari
80, watafanya operesheni
eneo la Vikindu na siwezi
kutaja idadi ya waliokufa
wala waliokamatwa, kwani
nitaharibu oparesheni. Idadi
kamili tutaitoa Jumanne
(keshokutwa),ííalisema.
Mapambano hayo
yaliyoanza juzi, katika eneo
hilo, ni moja ya juhudi za
polisi katika kukabiliana na
majambazi, ambao katika siku
za hivi karibuni wamefanya
matukio tofauti ya uporaji na
mauaji.
Tukio la karibu zaidi ni
lille lilitokea katika Benki
ya CRDB, Tawi la Mbade,
Dar es Salaam, ambako
waliwavamia na kuwaua
polisi wanne, kupora silaha
na kuharibu gari la jeshi hilo.
Akizungumzia kuhusu
maandamano yaliyopangwa
kufanywa na CHADEMA,
Septemba Mosi, mwaka huu,
Kamishna Sirro alisema tayari
wamepata taarifa kwamba,
kuna viongozi wazito
wameanza kumwaga fedha
kwa vijana ili kuwahamasisha
washiriki.
Kamishna Sirro alisema
taarifa za kiintelejensia
zinaonyesha kwamba,
viongozi hao wamekuwa
wakigawa sh. 40,000, kwa kila
kijana ili kuwapa hamasa ya
kushiriki maandamano hayo
yaliyopigwa marufuku na
serikali.
Sirro aliwataka vijana
wapenda amani, kutokubali
kuingia kwenye matatizo kwa
kuwa polisi wamejipanga
vizuri kukabiliana na
watakaokaidi marufuku
iliyotolewa na serikali kupitia
Jeshi la Polisi.
“Nawaomba vijana
wapenda amani, wasikubali
kuingia barabarani na
kushirikiana na wavunja
sheria kwa sababu
tutawashughulikia. Wapo
wenye uchu wa fedha,
watakaoshawishika kuingia
mtaani, msiungane nao.
Watambue kwamba,
wakiandamana, wanaweza
kuvunjwa mguu na fedha
hizo zisiwasaidie,”alisema.

No comments:

Post a Comment