Monday, 10 July 2017

BREAKING NEWSSSSS...HALIMA MDEE AFIKISHWA MAHAKAMANI KISUTU



MBUNGE wa Kawe, Halima Mdee (CHADEMA), amefikishwa kwenye Mahakama ya Kisutu, Dar es Salaam, leo asubuhi baada ya kuwekwa ndani kwa zaidi ya saa 48.

Mdee alikamatwa na polisi wiki iliyopita kwa amri ya Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Salum Happi, baada ya kudaiwa kutoa lugha chafu kwa Rais Dk. John Magufuli.

Mbali na amri hiyo, Hapi aliliagiza jeshi la polisi kumfikisha mahakamani mbunge huyo kwa tuhuma za kutoa lugha chafu dhidi ya kiongozi wa nchi.

Taarifa zaidi kuhusu kesi inayomkabili Halima tutawaletea baadaye.


No comments:

Post a Comment