Tuesday, 1 September 2015

DK. MAGUFULI ANATOSHA KUWA RAIS- DK. NCHIMBI

Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCm Dk. Emmanuel Nchimbi akihutubia wakazi wa Songea mjini ambapo aliwataka wananchi hao kumpa kura nyingi Mgombea wa Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM)Dk. John Pombe Magufuli kwenye uchaguzi utakaofanyika Oktoba 25.
Waziri wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi ambaye pia ni mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa Ndugu William Lukuvi akihutubia wakazi wa Songea mjini kwenye mkutano wa kampeni za CCM uliofanyika kwenye uwanja wa Maji Maji.
Mwigulu Nchemba akihutubia wakazi wa Songea mjini na kutaka wasihadahike na watu wenye uroho wa madaraka .
MGOMBEA urais kwa tiketi ya CCM, Dk. John Magufuli akihutubia mkutano wa hadhara kwenye Uwanja wa Majimaji, Songea

Na Mwandishi Wetu

MJUMBE wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, Dk. Emmanuel Nchimbi amesema Watanzania wanahitaji rais na sio mfano wa rais.

Amesema anao ushahidi wa kutosha kwamba mgombea urais wa CCM, Dk. John Magufuli ndiye anayestahili kuwa Rais wa Tanzania wa awamu ya tano.

Dk. Nchimbi alisema hayo jana wakati akiwasalimia maelfu ya wananchi wa mji wa Songea waliofurika kwenye Uwanja wa Majimaji katika mkutano wa hadhara wa kampeni za uchaguzi.

Alisema anao ushahidi wa kutosha kwamba Dk. Magufuli ametekeleza ahadi zake, hivyo Watanzania wanahitaji rais mwenye kutimiza ahadi.

Dk. Nchimbi aliwaonya wananchi wote wa mkoa wa Ruvuma wampigie kura Dk. Magufuli ili ashinde na kuwa rais.

AJIRA ASILIMIA 40
Akihutubia wananchi waliofurika katika Uwanja wa Majimaji, alisema iwapo atachaguliwa kuwa rais, ataongeza ajira kwa asilimia 40 kupitia sekta ya viwanda.

Alisema atatumia wawekezaji wa ndani na nje kujenga viwanda vikubwa, vya kati na vidogo, ambavyo vitaongeza uzalishaji na kuongeza ajira.

Dk. Magufuli alisema serikali yake itafanya kazi kwa karibu na wafanyabiashara wakubwa na wadogo ili kupata makusanyo halali ya kodi.

Alisema kupitia wafanyabiashara hao, fursa za ajira ndipo zitapatikana na kwamba serikali itakusanya mapato na kuyatumia kwa malengo yaliyokusudiwa, ikiwemo maendeleo ya wananchi.

Katika hatua nyingine, Dk. Magufuli amewatahadharisha wanaopora ardhi ya wananchi kiholela bila kuwalipa chochote kinyume cha sheria za ardhi, mipango miji na matumizi bora ya ardhi.

"Natambua kwamba kuna wananchi walioporwa eneo la EPZ. Sheria zinasema ukichukua eneo la mtu kama umemkuta, inabidi alipwe kwanza. Najua waliochukua eneo hilo wanasikia na ninajua wanaomba nisiwe rais, lakini kwa bahati nzuri wananchi wameshaamua mimi ndiye rais wa awamu ya tano,"alisema.

Pia alisema atatatua changamoto za wakulima za pembejeo, bei za mazao na barabara, hivyo atahakikisha anazifanyia kazi ili wakulima wafanyekazi na wapate fedha kwa wakati na sio kukopwa.

No comments:

Post a Comment