Tuesday 8 September 2015

KINANA: JIEPUSHENI NA MIGOGORO




NA SHAABAN MDOE, ARUSHA
KATIBU Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, amewataka wanasiasa hususani wabunge na madiwani, kuacha kusababisha migogoro ndani ya Chama baada ya kumalizika kwa kura za maoni.
Kinana alisema hayo jana alipokuwa akizungumza katika harambee ya kuchangia fedha za uchaguzi wa rais, mbunge na madiwani wa jimbo la Arusha Mjini.
Alisema sehemu nyingi za nchi katika majimbo mbalimbali, Chama kimepatwa na matatizo yaliyotokana na kura za maoni, ambapo wagombea wengi walioanguka katika kura hizo walifikia hatua ya kukata rufaa na hata kukihama Chama.
"Siku zote mwanasiasa mzuri ni yule anayetambua wakati wa kuingia na kutoka kwenye siasa bila kusubiri kusukumwa nje ya mfumo hali inayomwondolea heshima kwenye jamii," alisema.
 Alisema kutokana na baadhi ya wanasiasa kutotambua nyakati, kunawafanya wajiamini kuwa wanakubalika katika majimbo na kata zao bila kusoma alama za nyakati.
Kinana alisema wakati mzuri wa mwanasiasa kuachana na siasa hususan za ubunge na udiwani ni ule ambao bado wananchi na wanachama wanampenda na kumuhitaji, badala ya kusubiri wamchoke hadi kumtupa nje ya mfumo wa kisiasa na kupoteza heshima.
Alimtaka mgombea ubunge wa Arusha Mjini kukalia kiti hicho kwa kutafakari hayo iwapo atachaguliwa.

No comments:

Post a Comment