Tuesday 8 September 2015

MGOMBEA WA CUF APINGWA Z'BAR





Na Mwandishi Wetu
MGOMBEA Uwakilishi wa Chukwani kwa tiketi ya CUF, Mansour Yussuf Himid, amewekewa pingamizi kuwa hastahili kugombea uongozi kutokana na kosa la kukamatwa na silaha.
Mansour, ambaye ni mshauri wa karibu wa Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Shariff Hamad, alitimuliwa CCM kutokana na kwenda kinyume na maadili na taratibu za Chama, amewekewa pingamizi na Mwanaasha Khamis Juma, ambaye anawania jimbo hilo.
Akizungumza na waandishi wa habari jana, Ofisa wa Tume ya Uchaguzi  Zanzibar (ZEC), Suluhu Rashid, alisema wamepokea pingamizi dhidi ya Mansour na kwamba, inafanyiwa kazi kwa sasa.
Alisema pingamizi hilo na mengine mengi, yanafanyiwa kazi na uamuzi wa haki utatolewa kabla ya wahusika kuanza kampeni.
“Tumepokea pingamizi mbali mbali kutoka kwa wagombea uwakilishi na wabunge na sasa tunakusanya vielelezo na tutatoa uamuzi baadaye,” alisema.
Katika maelezo ya pingamizi hilo, inadaiwa Mansour hakuandika taarifa sahihi katika fomu za kugombea kuhusiana na mashitaka aliyowahi kushitakiwa katika Mahakama Kuu ya Zanzibar.
Aidha, anadai Mansour amedanganya juu ya maelezo ya kiapo cha Mahakama Kuu hivyo, amepoteza sifa za kuwa mgombea.
Katika maelezo hayo, Mwanaisha ameonyesha kuwa Mansour ameshitakiwa kwa makosa matatu ya kupatikana na silaha na risasi kinyume na sheria.
00000

No comments:

Post a Comment