Mbunge wa zamani wa Jimbo la Mchinga, Mudhihir Mudhihir akihutubia katika mkutano wa kampeni uliofanyika leo katika jimbo hilo mkoani Lindi |
Mbunge wa zamani wa Mchinga,Muhdhihir Mudhihir akiteta jambo na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Lindi Mzee Mtopa katika mkuano wa kampeni uliofanyika katika jimbo hilo |
MBUNGE wa zamani
wa jimbo la Mchinga (CCM), Mudhihir Mudhihir, amesema hana mpango wa kujiunga
na Ukawa, licha ya kuombwa na vigogo wake.
Mudhihir alisema
Ukawa walimfuata wakimtaka kujiunga na CUF ili kuitoa madarakani CCM katika
uchaguzi mkuu ujao, lakini hakuwasikiliza kwa kuwa ni wababaishaji.
Alifichua siri
hiyo jana katika mkutano wa kampeni uliofanyika Jimbo la Mchinga mkoani Lindi.
Alisema viongozi
wa kundi hilo walimfuata na alikataa ombi hilo kwa kuwa CCM ni chama madhubuti
kinachotekeleza vyema ilani ya uchaguzi.
Aliwataka watu
wanaoeneza uvumi kuwa ameihama CCM, kupuuzwa kwa kuwa hana mpango wa kujiunga
na UKAWA inayoongozwa na viongozi wabovu.
“Ukawa walinifuata
nijiunge nao, siwezi kufanya upuuzi wa aina hiyo…CCM ndio chama ambacho
kimenilea, siwezi kuwafuata watu wasiokuwa na dira,” alisema Mudhihir.
Aliongeza kuwa CCM
imeleta maendeleo makubwa nchini na kuwashangaa viongozi wa UKAWA wanaodai
hakuna jambo lolote lililofanyika.
Mudhihir,
ambaye amewahi kuwa Naibu Waziri, aliwashambulia Lowassa na Sumaye kuwa
viongozi waliokosa shukurani baada ya kulelewa na CCM.
“Mlinitaka
nije siji ng'o! Halafu Lowassa na Sumaye watu wa ajabu sana, wanadai CCM haijafanya
kitu wakati wao walikuwa mawaziri wakuu,” alisema Mudhihir.
Alisema wakazi
wa Mchinga wamepiga hatua na alitolea mfano wa kuongezeka kwa shule za msingi,
usafiri na miundombinu na kuwaasa kumchagua Dk. Magufuli na wagombea wengine wa
CCM.
No comments:
Post a Comment