Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa Muleba Kusini |
Helkopta iliyombeba Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana ikipasua anga la mji wa Bukoba. |
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa Bukoba kwenye mkutano wa kampeni za kuwanadi wagombea wa CCM kuanzia ngazi ya Urais, Ubunge na Udiwani |
NA PETER KATULANDA, Mwanza
KATIBU Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, amesema mabadiliko na maendeleo ya kweli yataletwa na mgombea urais wa CCM, Dk. John Magufuli.
Pia amewaasa kuachana na kuyapuuza mazingaombwe ya mgombea urais wa CHADEMA, Edward Lowassa, ambaye anatuhumiwa kwa kashfa mbalimbali.
Amesema mtu aliyekaa CCM miaka 40 na serikalini zaidi ya miaka 30 kisha akaiba fedha na kupora ardhi ya wanyonge, kamwe hatoweza kuwaletea Watanzania mabadiliko.
Kinana aliyasema hayo juzi jioni wakati akihutubia mikutano ya kampeni kwenye majimbo ya Sengerema, Magu na Ukerewe kuwanadi wagombea ubunge na madiwani.
Alisema genge la UKAWA na mgombea wao, wanatafuta visingizio vya kuwadanganya wananchi kwa sababu wanafahamu wameshashindwa kwenye uchaguzi mkuu.
Alisema kauli ya viongozi wa UKAWA kuwataka wafuasi kulinda kura ni ishara ya kushindwa hivyo, kutafuta visingizio vya ajabu ajabu.
“Ndani ya chumba cha kupigia kura CCM ina mtu mmoja, lakini wapinzani wako wengi ambao wote wanaiangalia CCM, kura zitaibiwaje. Wanataka kuwaacha juani kwa kutoa visingizo,” alisema huku akishangiliwa na umati wa watu.
Alielezwa kushangazwa na UKAWA kutoingiza ajaneda ya ufisadia kwenye mikutano yake ya kampeni wakati walikuwa wakiituhumu CCM kwa kuwatetea mafisadi, lakini baada ya chama kuwatema wamekuwa wa kwanza kuwakumbatia.
“CCM tunapofanya makosa tuna utaratibu wa kujikosoa, kumleta Magufuli ni sehemu ya kujikosoa ingekuwa ni utajiri, fedha, udini na umaarufu Magufuli angepita?
“Kama Lowassa anauchukia umasikini asingeiba fedha za wananchi na kujilimbikizia ardhi. Mabadiliko hayaji kwa mazingaombwe,” alisisitiza.
AVUNJA MKUTANO WA ACT
Wakati Kinana akiendelea na mikutano hiyo, mgombea ubunge wa ACT Wazalendo jimbo la Nyamagana, Chacha Okong’o, amelazimika kuvunja mkutano wake baada ya kukosa watu.
Akong’o, alipata pigo hilo baada ya mkutano wake wa kampeni uliokua ufanyike eneo la Dampo Kata ya Milongo, kukosa wananchi wa kumsikiliza.
Mgombea huyo wa ACT alilazimika kuwahutubia idadi ndogo ya wafuasi wa chama hicho wasiozidi 20 kufuatia wananchi kwenda kuhudhuria mkutano wa Kinana.
No comments:
Post a Comment