Thursday 19 November 2015

BEAKING NEWSSSSS......KASSIM MAJALIWA WAZIRI MKUU MPYA, WABUNGE WAMTHIBITISHA KWA KURA NYINGI, KUAPISHWA LEO JIONI


HATIMAYE Rais Dk. Johm Magufuli amemteua mbunge wa Ruangwa, Kassim Majaliwa Kassim kuwa waziri mkuu wa serikali ya awamu ya tano.

Rais Magufuli alikabidhi jina la mteule hiyo kwa Spika wa Bunge, Job Ndugai, ambaye naye alilitangaza kwa wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Mara baada ya Spika Ndugai kutangaza jina hilo kwa wabunge, bunge lilipuka mayowe ya kushangilia uteuzi huo.

Kwa mujibu wa kanuni za bunge, baada ya jina hilo kutangazwa, wabunge walilazimika kupiga kura kwa ajili ya kuidhinisha uteuzi huo.

Idadi kamili ya wabunge wanaotakiwa kuwepo bungeni ni 394, waliosajiliwa ni 369, lakini waliopiga kura ya kuthibitisha jina hilo walikuwa 351.

Akitangaza matokeo ya kura hizo, Katibu wa Bunge, Dk. Thomas Kashililah alisema kura zilizoharibika zilikuwa mbili, sawa na asilimia 0.06, zilizosema hapana zilikuwa 91, sawa na asilimia 25 na zilizosema ndio zilikuwa 258, sawa na asilimia 73.5.

Kutokana na matokeo hayo na kwa mujibu wa kanuni za bunge, Spika Ndugai alimtangaza rasmi Kassim Majaliwa kuwa waziri mkuu mpya wa serikali ya awamu ya tano.

Hafla ya kumuapisha Majaliwa inatarajiwa kufanyika jioni leo kwenye viwanja vya Ikulu Ndogo ya Chamwino mjini Dodoma.

Wakati huo huo, wabunge leo asubuhi wamepiga kura ya kumchagua Naibu Spika wa Bunge.

Waliokuwa wakichuana katika kinyang'anyiro hicho ni mbunge wa kuteuliwa Dk. Tulia Ackson wa CCM na mbunge wa Urambo Magharibi kwa tiketi ya CUF, Magdalena Sakaya.

Hata hivyo, Dk. Tulia ndiye anayepewa nafasi kubwa ya kuibuka mshindi kutokana na CCM kuwa na idadi kubwa ya wabunge ikilinganishwa na wapinzani.

No comments:

Post a Comment