Waziri wa Kilimo, Uvuvi na Ufugaji, Mwigulu Nchemba akiangalia ng'ombe walio uwawa katika mgogoro wa wakulima na wafugaji uliotokea katika kijiji cha Dihinda kata ya Kanga wilayani Mvomero, katika tukio lililotokea Desemba 12 mwaka huu.
Waziri wa Kilimo, Uvuvi na Ufugaji, Mwigulu Nchemba akiwa na Mkuu wa wilaya ya Mvomero, Betty Mkwasa wakiwajulia hali watu waliojeruhiwa katika mgogoro wa wakulima na wafugaji uliotokea katika kijiji cha Dihinda kata ya Kanga wilayani Mvomero Desemba 12 mwaka huu.
Waziri wa Kilimo, Uvuvi na Ufugaji, Mwiguku Nchemba amemwagiza Mkuu wa Wilaya ya Mvomero, Beth Mkwasa kuunda kamati ya Ulinzi na Usalama katika wilaya ya Mvomero ili ihusike maeneo yote ya nchi ili kuhakikisha wanaimarisha ulinzi maeneo yote yenye migogoro. Pia amewataka wahakikishe waliosababisha maafa wanakamatwa mara moja na kufikishwa kwenye vyombo vya sharia.
"Natoa rai kwa wananchi hususani wa jamii ya Wafugaji na Wakulima, kuwa hakuna ardhi au Mnyama mwenye thamani sawa na maisha ya mwanadamu yeyote yule, njia bora na salama ya kutatua migogoro hii inayohusisha wakuliama na wafugaji ni kufuata taratibu za kuonana na uongozi wa serikali wa eneo husika hatua kwa hatua. Nawaomba wananchi waache kujichukulia sheria mikononi, tunakwenda kuunda kamati za usuruhishi wa migogoro hii kwa kila kijiji zitakazohusisha pande zote mbili ili kubaini wavamizi wa maeneo na kuwachukulia hatua za kisheria," alisema Nchemba.

No comments:
Post a Comment